Breaking News

Your Ad Spot

Sep 2, 2012

MWANDISHI WA CHANEL TEN AUAWA IRINGA KATIKA VURUGU ZA CHADEMA NA POLISI

Mwandishi wa habari wa Kituo Cha Televisheni cha Channel Ten,  Daudi Mwanagosi amekufa katika vurugu nyingine za Chadema na Polisi zilizotokea leo, eneo la Nyololo mkoani Iringa.
      
Habari zilizothibitishwa na polisi zimesema, mwangosi amefariki baada ya patashika la vurugu baada ya Chadema kujaribu kufanya maanfamano ambayo polisi ilikuwa imekataa yasifanyike.

Kwa mujibu wa habari hizo, Wakati polisi waliporusha mapomu ya machozi inadaiwa mwandishi huyo alipatwa na dhoruba na kuumua sehemu za tumbo hatua iliyomsababishia kifo.

Kifo cha Mwandishi huyo kimekuja zikiwa ni siku chache tu zimepita tangu mtu mwingine mmoja muuza magazeti, kufariki dunia kwa kinachodaiwa kupigwa risasi, baada ya vurugu za Chadema na Polisi mjini Morogoro. Cha kushangaza ni  kwa nini  kwenye maandamano vurugu hizo waliodhuriwa ni watu wa kada tofauti na siyo wanasiasa au wafuasi wa vyama vya siasa wanaokuwa kwenye maandamano yanayokuwa yanazuiwa na hivyo kuzusha vujo.

2 comments:

  1. HIVI HII DEMOKRASIA TUMEIPOKEAJE, MBONA INAKUWA KAMA SUMU NYINGINE YA KUTUMALIZA KIDOGO KIDOGO, AU HATUJAIELEWA VYEMA? Mimi kwa mtizamo wangu, labda tungelikuwa na aina fulani ya siasa ya kikwetu, tukaiita AFRIKASIA!

    ReplyDelete
  2. Nimekua nikifuatilia sana kuhusu mikutano ya CDM na matokeo ya mikutano hiyo ni vurugu zisizo na maana na kusababisha mapambano na vyombo vya dola kwa kukaidi amri halali zitolewazo na vyombo vya usalama na kusababisha vifo.. hivi ni kwa nini viongozi wa CDM kwa makusudi wamekua wakiyayafanya haya bila kuchukuliwa hatua za kisheria?na ni kwa nini wanasafiri na makundi ya vijana toka mkoa mmoja kwenda mwingine kwa ajili ya kutaka mikutano yao ionekane kujaa?? naomba mamlaka husika zichukue hatua za tahadhari kabla ya kidonda ndugu hiki kufikia hatua ya kutopona na kuleta madhara makubwa ya umwagaji damu.

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages