Breaking News

Your Ad Spot

Oct 9, 2012

HOJA MTAMBUKA


NEC IMEFANYA MAAMUZI SAHIHI KWA MANUFAA YA CCM NA TAIFA
NA TAMBWE HIZA (PICHANI)
Katika gazeti moja litolewalo kila siku toleo la juzi lilimnukuu Mzee Wilbraod Slaa akiponda maamuzi ya Halmashauri kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi kwa kuwapitisha wanachama wake wakongwe Edward Lowasa na Andrew Chenge kugombea Ujumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa katika Wilaya zao (Monduli na Bariadi).
Jambo alilofanya Slaa kwa Hakika halikushangaza sana kwa kuwa ni hulka ya viongozi wa Chadema kutokubaliana na maamuzi yeyote yanayomhusisha Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kutaka kujaribu kuonyesha kwamba yeye binafsi na CCM yake haiko makini.
Inajulikana,hili analifanya kwa kutambua vikao vyote muhimu kuanzia kile cha maadili, Kamati kuu na NEC vyote viliongozwa na Mh. Kikwete, tangu hatua ya kupitia mapendekezo ya ngazi za chini na hatimaye kupitisha wagombea walioonekana wanafaa,hapo ndipo Slaa akaona atumie nafasi hiyo kuendeleza utovu  wa nidhamu na ushindani ambao hautokuwepo tena kati yao kwa kuwa kikwete hatagombea tena urais, na kikao kizima cha Halmashauri kuu ya Taifa.
Sababu alizotoa dhidi ya maamuzi ya NEC hazina uzito wowote wala chembe ya ushahidi wa kitafiti zaidi ya fikra zake binafsi,sababu aliyotoa inayohusiana na shutuma alizozianzisha yeye na chama chake dhidi ya Chenge na Lowasa hazina uzito wowote wala chembe ya ushahidi wa kitafiti unaothibitisha CCM ikiwapitisha wanachama wake hao kugombea u-NEC itapungua nguvu mbele ya Umma ,Mzee Slaa anasahau kwamba shutuma hizo ni yeye na chama chake ndiyo walio zianzisha siku nyingi na kufikiri zitawasaidia kushinda uchaguzi Mkuu uliopita, hazikuwasaidia , walianguka vibaya kwa kupata viti 23 vya ubunge katika majimbo 239,CCM ikiibuka kidedea na viti 186, CUF 24,NCCR 4,TLP 1 na UDP 1,kwa upande wa Madiwani waliambulia viti 326 (9.8%) CCM ikipata 2,803 (84%) kati ya viti 3,335,Urais  Kikwete 61% dhidi ya Slaa 26%.
Tukizingatia kwamba madiwani ndiyo wapo karibu zaidi na wananchi idadi hiyo ya ushindi wa CCM inathibitisha jinsi chama kinavyokubalika na  ukaribu wake kwa wananchi 
Mzee Slaa anapaswa kuelewa waheshimiwa Chenge na Lowasa walishinda kwa kishindo kikubwa katika Majimbo yao ya uchaguzi (Lowasa   % na Chenge    %) mbali ya shutuma hizo nzito kutoka kwa wapinzani sasa hoja yake hiyo anaisimamisha katika vigezo gani?
Isingekuwa haki au busara kwa CCM kuwazuia kugombea kwa tuhuma za kisiasa zinazoenezwa na wapinzani wake wa kisiasa ambazo hazijathibitishwa na chombo chochote cha kisheria,ukisoma vizuri Anserd za bunge utaona kamati ya Bunge kuhusu Richmond hakuna mahali popote ilipomtia hatiani Lowasa, Slaa alikuwa Mbunge na analijua hili vizuri, kuhusu Chenge  sfo ya uingereza imeshatoa taarifa za kumsafisha baada ya kukamilisha uchunguzi wake kwa nini aendelee kumtuhumu?, CCM ni chama cha Kidemokrasia kimewaachia wananchi wa Wilaya zao kufanya maamuzi, zingekuwepo sababu nyingine zozote za msingi CCM isinge sita kuwatosa kama ilivyowahi kufanya hivyo mara nyingi kwa wanachama mbalimbali bila kujali madaraka na umaarufu wao.
slaa anapaswa kuelewa kama tuhuma pekee zinatosha kuondoa sifa mtu ya kuwa kiongozi yeye asingekuwemo katika ulingo wa siasa kwa tuhuma zilizoko mbele yake kutokua mwaminifu katika kanisa kwa kuwa Mkware (Padri Mwenye Mpenzi na watoto),kesi aliyofunguliwa na Mzazi mwenzake (Rose Kamili)Mahakamani, kuchukua mke wa mtu,Ubadhirifu wa Fesha za TEC wakati wa ujio wa PAPA hapa nchini uliopelekea kuundwa kwa Tume ya father Moreka na hatimaye kuondolewa katika nafasi zake zote za kanisa 
Mambo ya ndani ya vyama kila chama kiachiwe kifanye chenyewe,CHADEMA haiwezi kuhimili kishindo cha kuingiliwa mambo yake ya ndani na CCM hivyo ni bora isiichikoze asubiri uchaguzi ashindwe tena

1 comment:

  1. Hawa jamaa hatari kweli wanauwezo mkubwa kugeuzageuza maneno ili kujenga uhalali wa anachokijengea hoja kwa wakati huo.

    Hivi uzee ni dhambi? na je katika chama anachokiongoza hakuna viongozi wazee?

    Binafsi sina uhakika lakini kwa mtazamo wangu hata yeye SLAA ni mzee vilevile.

    Tena anafanya kazi ya kuajiriwa kama Katibu Mkuu. Afahamu U NEC siyo ajira ni uongozi tena wakuchaguliwa cha muhimu awaachie wajumbe wataamua

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages