Breaking News

Your Ad Spot

Oct 9, 2012

ASHA ABDALLAH JUMA 'MSHUA' APETA BARAZA KUU LA UWT

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na katibu wa  NEC Oganizesheni Bi Asha Abdalla Juma, alipokuwa akijieleza katika Uchaguzi wa UWT Mkoa wa Mjini ,uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Amani juzi,katika uchaguzi huo Bi Asha aliibuka kuwa mshindi wa pili utamuweweza kushiriki katika  Baraza Kuu Taifa la UWT.
 Baadhi ya wapiga kura wa kuwachagua wajumbe wa UWT Mkoa wa Mjini akisherehekea  ushindi wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na katibu wa  Nec Oganizesheni Bi Asha Abdalla Juma, baada ya kuibuka kuwa mshindi wa pili katika wanachama waliowania nafasi hiyo zaidi ya kumi, katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Amani juzi

Picha ya pamoja ya wanachama  wa CCM waliowania nafasi ya Baraza Kuu la UWT kabla ya kujieleza kila mmoja katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Amani juzi, {Picha zote kwa hisani ya Mwarabu Mmadi}

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages