Breaking News

Your Ad Spot

Oct 1, 2012

MELI MPYA YA KISASA YA AZAM MARINE YENYE UWEZO WA KUBEBA ZAIDI YA WATU 1000 NA MAGARI 200 YAWASILI NCHINI


Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visawani Zanzibar kwa mara kwanza.

Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli hiyo iliyowasili Visiwani Zanzibar leo.
Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.
Sehemu ya Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.
Muonekano wa ndani wa Lounge ya kumpzikia wasafiri.
Muonekano wa nje. (Picha na Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.
Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali.
Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.
Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari.
Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.
Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.
Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages