Breaking News

Your Ad Spot

Oct 7, 2012

MKUTANO WA CHADEMA WAKOSA WATU ARUSHA


Ni baada ya wengi kuchangamkia wa uzinduzi kampeni za CCM
ARUSHA, TANZANIA
UZINDUZI wa kampenzi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Daraja mbili jijini Arusha umesababisha mahudhurio hafifu ya wananchi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chadema uliofanyika eneo la jirani na mkutano wa CCM.

Mkutano wa CCM ulifanyika eneo la Lamlawa wakati ule wa Chadema ulifanyika eneo la Sokoni 2 jirani kabisa na eneo la mkutano wa CCM.

Mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano wa CCM Mwamvita Gulugwa alisema wengi wa wananchi walisusia kwenda katika mkutano wa Chadema kutokana kuhofia vurugu kutokana na kubadilisha badilisha tarehe zao za uzinduzi ili kufungana na CCM.

Alisema awali chama hicho kilitangaza kufanya uzinduzi wa kampeni zake siku ya Oktoba 3 ambapo CCM kilitangaza kufanya uzinduzi wake Oktoba 6 lakini cha kushangaza Chadema kilianza kubadilisha kwenda Oktoba 7 na baadae kwenda Oktoba 6 sawa na CCM hali iliyowatia wasiwasi kwakua ni chama cha vurugu.

Hata hivyo mwandishi wa gazeti hili aliyeshuhudia hiyo na kumuhoji wananchi hao walisema hali hiyo imetokana na wananchi wengine kuhofia vurugu kwakua hizo zilikua ni dalili za kutafuta vurugu pamoja na kukosekana kwa sera mpya.

Awali akizindua kampeni hizo mwenyekiti mpya wa CCM wilaya ya Arusha Dk.Wilfred Soilel aliwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua Phillip Mushi katika nafasi hiyo ili aweze kukamilisha miradi iliyoaachwa na aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu,Bashiri Msangi.

Dk.Soilel alisema mgombea huyo wa CCM ni mtu anayekubalika na ndie atakawezesha kukamilika kwa miradi mbalimbali ya maendeleo na kazi yake ni ubunifu.

Aliwataka wanachama wa CCM,kutojibizana mitaani na vyama vya kisiasa bali majibizano yafanyike kwa kumchagua,Mushi,kuwa diwani wa kata hiyo ili aweze kukamilisha miradi iliyobakia na  kuwaondolea wananchi kero.

Nae mgombea huyo amewahakikishia wananchi kusimamia changamoto za ukamilishaji wa miradi mbalimbali inayoikabili kata hiyo ikiwemo ujenzi wa Zahanati na ukarabati wa bara bara,kuendeleza ujenzi wa shule ya sekondari ya khiyo kuwa ni ya gharofa na kuandika historia kuwa ni kata ya kwanza jijini Arusha kuwa na shule ya ghorofa.


Alisema changamoto zingine zilizopo katika kata hiyo ni kuongeza vyumba vya madarasa katika shule ya msindi Daraja mbili kutoka 28 ili vitosheleze mahitaji. 

Kuhusu ukosefu wa ajira amesema hilo ni tatizo la dunia nzima hivyo akaahidi  kuanzisha vikundi vya vijana 25 kila mtaa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa kufyatua tofari,kuwatafutia mitaji akina mama kupitia Saccos kutokana na kutokuwa na mitaji na kuwataka waachane na malumbano ya vyama vya kisiasa kwa sababu hayana tija.

Alisema iwapo atachaguliwa atawahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi wa itikadi ya kisiasa wala dini kwa sababu yeye atakuwa ni kiongozi wa wote.

Kwa upande wake mstahiki Meya,wa Jiji la Arusha,Gaudensi Lyimo,aliwaomba wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea huyo ili aweze kuhudhuria kwenye vikao vya baraza la madiwani ambavyo ndivyo  vyenye maamuzi ndani ya halmashauri na kero zao zitapatiwa ufumbuzi.kwa faida ya wananchi.

Alisema madiwani wa Chadema wapo katika mgomo wa kutoingia baraza la madiwani kutokana na maelekezo ya viongozi wao wa juu ambapo matokeo yake ni kukwamisha  wananchi jambo ambalo ni tofauti na ahadi zao  na pia linaenda kinyumne na demokrasia.

Alisema iwapo watamchagua diwani ambae hahudhurii vikao ni sawa na kazi bure kwakua hawatakua na mwawakilishi katika vikao vya baraza la madiwani na kukosa mtu wa kuwasemea kuhusu kero zilizopo katika kata yao. 

Nae mwenyekiti wa mtaa wa Ally Nyanya,Omar Sheh,amevionya vyama vya kisiasa kutokuthubutu kuchoma bendera za CCM,katika kata hiyo kama vinavyojinasibu,na akawakumbusha kuwa kinachotakiwa ni maendeleo na sio vurugu.

Alisema wakithubuti kuchoma bendera ya CCM,katika kata hiyo kama wanavyojinasibu watambue kuwa mwisho wao umefika atawasaka mmoja mmoja mpaka kieleweke kwa sababu anawafahamu wote.

Uchaguzi huo pamoja na ule wa kata ya Bangata wilayani Arumeru unatarajiwa kufanyika mnamo Oktoba 28 mwaka huu ili kumpata madiwani watakayeshika nafasi zilizoachwa wazi na madiwani wa CCM baada ya kufariki dunia.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages