Breaking News

Your Ad Spot

Oct 7, 2012

SHY ROSE ABWAGWA UJUMBE WA BARAZA KUU UWT TAIFA


MUSOMA,TANZANIA 
MBUNGE wa Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji amebwagwa katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi wa Ujumbe Baraza Kuu la UWT Taifa, kuwakilisha kina Mama kutoka Mkoa wa Mara baada ya kushindwa na mjasiliamali mdogo, Agness Mathew aliyepata kura 274, Shy-Rose akipata kura 249, kati ya kura 526 zilizopigwa. 

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi, Jackson Msome alisema alimtangaza Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mara kuwa ni Nancy Msafiri alipata kura za ndiyo 429 na kura 89 za hapana. 

Aliwatangaza wengine katika nafasi na kura zao zikiwa kwenye mabano kwa ya Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa, alipata Stellah Manyonyi(312), Mkutano Mkuu CCM Taifa, Amina Masenza aliyepata kura (273), na  nafasi ya kuwakilisha Wazazi Mkoa, Mercy Mollel alipata kura 195 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Rose Magoti, ambaye pia ni diwani wa viti Maalum (145).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages