Breaking News

Your Ad Spot

Nov 4, 2012

BRIDGITA KUTOKA SINZA ALITWAA TAJI LA MISS TANZANIA 2012

Bridgita na washindi wa Pili na Watatu baada ya kutwaa hilo.
Bridgit Alfred (18), kutoka Kitongoji cha Sinza 'Kwa Wajanja', Wilaya ya Kinondono mkoani Dar es Salaam,  ametwaa taji la Miss Tanzania 2012, katika shoo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Blue Pearl Hotel, uliopo ndani ya jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. 
   Kwa ushindi huo, amezoa zawadi ya kitita cha  Sh. Milioni 8 na gari ambalo thamani na aina yake vitajulikana baadaye, huku mshindi wa pili Euegene Fabian akijipatia zawadi nono ya Sh. Milioni 6.2 na wa tatu Eddah Sylvester kibunda cha sh. Milioni 4. Habari zaidi BOFYA HAPA kwenye Ukurasa wetu wa Spoti.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages