Mtayarishaji wa Daily Nkoromo Blog, Mimi ni mmojawa wasomaji wakubwa wa blogu yako hii ya jamii, hivyo kama mdau naomba unirushie haya maoni yangu ili wadau wenzangu waweze kuyasoma.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia baadhi ya vipindi vyenye mlengo wa kisiasa kwenye televisheni ya Star Tv, nimebaini kwamba baadhi ya vipindi hivyo ninaendehswa kupigia debe upinzani kama Chadema.
Mfano mada ya leo asubuhi ya 'Jicho letu ndani ya Habari' katika kipindi cha "TUONGEE ASUBUHI" chini ya mtangazaji Doto Bulendu, kimethibitisha hilo.
Kwanza, katika mjadala huo, wametumia makala kutoka gazeti la Tanzania Daima ambalo kwa wafuatiliaji wengi wa masuala ya siasa za Tanzania wanalifahamu mlengo wake, na kwa hivyo haliwezi kuandika makala inayosifia maendeleo yanayoletwa na serikali ya Rais Jakaya Kikwete chini ya CCM.
Kwa mujibu wa mjadala huo, ni kwamba Azimio la Arusha limeachwa na hivyo kusababisha ufujaji mali na rasilimali kwa kuwa hakuna mfumo wa kuwakataza kwa sababu Tanzania sasa haina Itikadi rasmi.
Nimewasikiliza sana mwanzo hadi mwisho, na nikajaribu kupiga simu nitoa maoni yangu lakini simu ikawa bize ingawa 'walengwa' walikuwa wanaipata.
Ukweli ni kwamba, tatizo siyo msingi wa itikadi bali usimamizi ndiyo tatizo linalokabili mfumo uliopo sasa.
Mfumo uliopo sasa kwa mtu mwenye kupenda kuukumbatia ukweli atakubali kwamba itikadi ya sasa ni ya manufaa kwa sababu imekuja kulingana na wakati tulio nao lakini tatizo ni usimamizi mbovu.
Wasio wabishi watakubaliana kwamba Watanzania wa sasa kama wataishi katika mfumo ule wa zamani, wa Ujamaa uliofuata miiko yote, lazima wangekuwa wanaadamana kila siku.
Watanzania wa siku hizi, naamini wasingevumilia, hali ile ninayoikumbuka wakati ule.
Hebu fikiria, wakati ule ilikuwa ni kosa mtu kukutwa umevaa nguo au viatu a.k.a raba mtoni kutoka nje ya nchi, ilikuwa kosa kukutwa unamiliki duka binafsi kwa sababu yalikuwepo maduka ya ushirika ambako ukitaka kununua mchele unalazimika kununua pia unga wa njano.
Kilikuwa kipindi ambacho kwa kweli lazima watanzania wa sasa wangeandamana. Kweli wapo Watanzania wa sasa ambao wangevumilia kupata huduma ya sukari, unga, sabuni na mchele kwa kupanga foleni ya mawe asubihi mapema kwenye duka la Kaya?
Kwenli wapo Watanzania wa sasa ambao wangeacha kuandamana katika maisha ya wakati huo, ya kulazimika kukimbiza lori la ugawaji hadi linakosimama ili kupata bidhaa hizo?
Mimi ni miongoni mwa Watanzania waliokuwepo wakati huo nikiwa na umri wa miaka kama 20 hivi. nakumbuka wakati huo, siku moja nilikamatwa na polisi hadi kituo cha Oysterbay baada ya kunikuta nimevaa viatu vya wazi vya platiki tulivyokuwa tunaviita Cha cha cha!
Nilipokutana na polisi eneo la Mwananyamala kwa Kopa, polisi wawili walinisimamisha kisha wakaniluliza, Aisee, viatu hivi umevipata wapi? nikawajibi nimevununua Madanda nchini Burundi.
Baada ya majibizano hayo wakanikamata na kunipeleka moja kwa moja kituo cha polisi cha Onysterbay ambako nilivuliwa na jinsi nilivyotoka huko hayasemeki.
Ni wakati ambao kwa kweli kwa wakati huo ulikuwa ukiwastahili Watanzania wa wakati ule, sio wa sasa ninaowajua.
Nakumbuka pale Kijitonyama wakati huo, kuna mtu aliyekuwa na gunia la maharage nyumbani kwake, lakini kwa hofu ya kukamatwa alilazimika kuyachimbia shimo barabarani akayafukia wapitanjia wakawa wanashangaa kuona yakiota kwa wingi.
Msifanye masihara, wakati huo ilikuwa kosa kuwa na Tv nyumbani. Nalkumbuka pale pale Kijitonyama, asubuhi moja nilikuta TV nzima kabisa zimetupwa kando na njia na mtu aliyehofu kukamatwa.
Kwa sababu ya kubaini madhila ya kimaisha kama hayo na mengne ambayo sikuyataja, nadhani ndiyo moja ya sababu zilizomfanya Rais wa awamu ya Pili, Ali Hassani Mwinyi kupitia Azimiao la Zanzibar kufungua milango la kiuchumi.
Ni kutokana na hali hiyo ndiyo zikapatikana fursa za kufungua vituo vya televisheni kama Star TV huku TV zikiwa bwerere kila nyumba bila hofu.
Kimsingi Changamoto zinazotokea sasa, siziungu mkono, lakini si changamoto katili kama zilizokuwepo kabla ya mfumo wa sasa, ni changamoto ambazo ufumbuzi wake utahitaji usimamizi tu na siyo kulalamika na kugeuzwa mtaji wa kisiasa hadi kwenye vituo vha televisheni.
Changamoto hizi naziona kuwa zinageuzwa mtaji wa kisiasa kwa sababu, ndizo zinazowapa fursa wanasiasa wa sasa kutamba hadi kujipenyeza katika vyombo vya habari kama hiyo Star TV.
Katika kipindi hicho cha leo, nimeshangazwa sana kuona kwamba, namba 0732 78 27 88 iliyokuwa ya watazamani kutoa maoni yao, ilikuwa bize kila ukipiga, lakini watu waliokuwa na maoni ya kushutumu ndio waliweza kuzungumza tu, jambo linalonilazimisha niwaze kwamba walipangwa watu maamlum wa kupata nafasi ya kupokewa simu zao.
MAONI HAYA YAMETUMWA NA RAMADHANI KILAMIAH SALUM, WA DODOMA; EMAIL: ramakilah@gmail.com, simu: 0773 600007.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269