Breaking News

Your Ad Spot

Nov 17, 2012

KUELEKEA KRISMAS NA MWAKA MPYA, SUMTARA YAAPA KUSHUGHULIKIA KIKAMILIFU WENEYE MABASI YATAKAYOPANDISHA NAULI HOVYO



DAR ES SALAAM, TANZANIA
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imepia mkwara ikisema itawakamata wamiliki wa magari watakaohusika katika kupandisha nauli hovyo wakati wa kuelekea sikukuu za Krismas na mwaka mpya.

Msemaji wa Mamlaka hiyo, David Mziray (Pichani)  amesema  jijini Dar es Salaam kwamba kuna taarifa kuwa kuna baadhi ya madereva na makondakta wameibua mbaya ya kupandisha nauli kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Alisema wamejipanga vizuri kwani wamewaandaa vijana watakaoshirikiana na Jeshi la Polisi ili kuzikamata kampuni za mabasi ambazo zitabainika kupandisha nauli kinyume cha sheria.

 Mziray alisema katika kipindi hiki wataendesha opresheni kila siku ya kukamata kampuni ambazo zitaenda kinyume na mkataba wao wa  leseni, itatozwa fani ya  sh 25000.

Sambamba na hilo, aliwatahadhalisha wamiliki wa magari hayo kuwa makini ili kuepuka kutozwa faini ambazo kwa kiasi kikubwa zinaumiza wao na wala siyo madereva na makondakta.

“Nafahamu kweli kuna baadhi ya magari hivi sasa yamekwishaanza kupandisha nauli kutokana na kuongezeka kwa abiria wanaosafiri kwenda kuungana na familia zao katika kipindi cha kusherehekea Sikukuu ya Krismas”alisema.

Mziray alisema SUMATRA haitasita kuzifutia leseni kampuni ambazo zitaonekana kuwa sugu katika kujiingiza kwenye vitendo hivyo vya kupandisha nauli kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuwaibia wananchi.

Vile vile aliwaasa abiria  kutoa ushirikiano katika operesheni hiyo ya kuzikamata kampuni zinazojihusisha na upandishaji huo wa nauli, wakati mwingine wanashindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na abiria wenyewe kuwa wagumu kuwafichua madereva na makondakta wanaofanya hivyo.

Hata hivyo,  Mziray alitoa wito kwa wananchi kupanga nasafari zao kwa utaratibu na wala siyo kurupuka kwani mara nyingi wale wanao kurupuka kwa kutaka kusafiri siku hiyo hiyo ndiyo maranyingi wanaokumbana na ubabaishaji huo katika kupata tiketi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages