Breaking News

Your Ad Spot

Nov 13, 2012

LIVE KUTOKA MKUTANO MKUU WA CCM, KIZOMA MKOANI DODOMA


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimia baadhi ya wana-CCM, wakati akiingia kwenye ukumbi wa Kizota, kuendesha Mkutano Mkuu wa CCM unaomalizika leo
 Msinisahau katika Ufalme wenu: Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimia baadhi ya wana-CCM, wakati akiingia kwenye ukumbi wa Kizota, kuendesha Mkutano Mkuu wa CCM unaomalizika leo. Kikwete anapigiwa kura leo ili kuweza kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.
 Msanii Vicky Kamata  akiimba wimbo maalum kunogesha Mkutano Mkuu wa CCM katika ukumbi wa Kizota, Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na meza kuu, wakishiriki kucheza wimbo maalum ulimbwa na Vicky Kamata kabla ya kuanza mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na meza kuu, wakishiriki kucheza wimbo maalum ulimbwa na Vicky Kamata kabla ya kuanza mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salim Ahmed Salim, wakifuatilia matukio kwenye mkutano huo, ukumbini.
 Wake wa viongozi ,Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Fatma Karume, Mama Kawawa, Shadya Karume, Mwanamwema Shein na Tunu Pinda wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wajumbe na waalikwa wakimiminika kuingia kwenye viwanja vya Kizota, Dodoma wakati wa mkutano mkuu leo
 BIASHARA: Wajumbe na waalikwa wakinunua bidhaa zinazouzwa na wajasiriamali nje ya ukumbi wa Kizota, Dodoma wakati wa mkutano huo.
 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Janeth Mbene akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya  Magu, Jacqueline Lina nje ya ukumbi wa Kizota.
  Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Janeth Mbene akizungumza na Kamanda Asas wa UVCCM, mkoa wa Iringa, nje ya ukumbi wa Kizota.
 Kamanda Asas wa UVCCM mkoa wa Iringa akitazama nakala ya UHURU alipotembelea banda la kampuni ya Uhuru Publications Ltd, wanaochapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, kwenye viwanja vya Kizota.
 Banda maalum la Mamalishe ndani ya viwanja vya Kizota
 Mtangazaji wa TBC Swedy Mwinyi, akiwa 'live' wakati wa mkutano mkuu wa  CCM, kwenye ukumbi wa Kizota, Dodoma, Kulia ni Swedy Mwinyi na Salum Othman wa Shirika la Utangazaji Zanzibar. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages