Breaking News

Your Ad Spot

Dec 22, 2012

AHUKUMIWA MIAKA KUMI JELA KWA KUMILIKI KOBE


MARA, Tanzania
JAMAA mmoja raia wa India, amehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela au kulipa faini ya sh. milioni 3.6, baada ya kukubali katika mahakama ya wilaya ya Bunda, mkoani Mara, kumiliki kobe kinyume cha sheria.

Aliyekumbwa na adhabu hiyo ambayo imetolewa na hakimu Safina Simfukwe, ni Kanchan Mitra (65), anayefanya kazi kwenye kampuni ya Kichina inayotengeneza barabara ya Mwanza-Musoma.

Awali mwanasheria wa hifadhi ya taifa ya Serengeti, Emmanuel Zumba, alisema kuwa mshitakiwa huyo alikamatwa Des 29, mwaka jana, akiwa na wanyama hao kwenye kambi ya kampuni ya kichina, iliyoko katika eneo la Sabasaba, wilayani Butiama.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa mshitakiwa huyo alilipa faini hiyo ya sh. 3,660,000 na kuachiwa huru

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages