Breaking News

Your Ad Spot

Dec 11, 2012

MAANDALIZI YA UTALII WA NDANI YAIVA

Mkurugenzi wa kampuni ya Lakeland Africa inayoratibu safari ya utalii wa ndani inayotarajiwa kuanza, wiki hii, Desemba 14, 2012, Silva Muniko akizungumzia maandalizi ya safari hiyo leo, jijini Dar es Salaam.
Lori maalum la utalii, lenye huduma muhimu ndani lililoandaliwa kutumika kwenye safari hiyo

Lori hilo linavyoonekana kwa ndani
Moja huduma zilizomo kwenye lori hilo ni pamoja na sehemu maalum ya kuchaji simu au kompyuta wakati wa safari



HABARI KAMILI

DAR ES SALAAM, TANZANIA
KAMPUNI ya Lakeland Africa imeandaa safari ya utalii wa ndani kwa ajili ya Watanzania inayotarajiwa kuanza Desemba 14, 2012 Ijumaa.
     Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Silvanus Muniko amesema leo kuwa, safari hiyo ya siku 14 itawashirikisha watalii wa ndani 24, ambao watasafiri kwa gari maalumu litakalokuwa na huduma zote muhimu.
     Silvanus alisema lengo la kuanzisha safari hizo za utalii wa ndani ni kuwawezesha Watanzania kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii kwa gharama nafuu.
Alisema katika safari hii ya kwanza, watanzania hao watatembelea vivuti 14 vya kitalii na watapata huduma ya chakula na malazi kwa siku zote 14.
     Kwa mujibu wa Silvanus, gharama ya safari hiyo kwa mtu mmoja ni sh. 1,500,000 kwa atakayesafiri kwa ndege kutoka Mwanza kurejea Dar es Salaam na sh. 1,300,000 kwa atakayeamua kurejea kwa gari litakalowasafirisha katika vivutio vyote.
     Alivitaja vivutio, ambavyo watanzania hao watatembelea kuwa ni Hifadhi ya Saadan, Pangani, Lushoto, Tarangile, Olduvai Gorge, Lake Manyara, Ngorongoro na Serengeti.
Silvanus alisema pia kuwa, watanzania hao watapata nafasi ya kutembelea kijiji cha Butiama alikozaliwa     Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere na kuzuru katika kaburi lake.
    Mkurugenzi huyo wa Lakeland Africa ametoa mwito kwa watanzania kujitokeza kushiriki katika safari hiyo ya kitalii ya siku 14 itakayoanza jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu hadi Desemba 27 mwaka huu.
“Kwako mtanzania sasa inawezekana kujua Tanzania yako, si lazima kuwa mzungu kuwa mtalii wa ndani,"alisema.
    Alisema gari litakalotumika kwa safari hiyo litakuwa na vifaa vya umeme (laptop, simu, kamera) kwa kila mtalii kuwa na soketi yake. Magari ambayo yamekuwa yakitumiwa na makampuni ya utalii katika nchi za ulaya sasa kutumika Tanzania pia.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages