Breaking News

Your Ad Spot

Dec 10, 2012

RAY APONA, AENDA IKULU KUMSHUKURU RAIS KIKWETE LEO


Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyewahi kuwa nyota hapa nchini, Rehema Chalamila, maarufu kwa jina la  'RAY C',   leo amefika Ikulu jijini Dar es Salaam, kumshukuru Dk.Jakaya Mrisho Kikwete, kumshukuru kwa msaada wa matibabu aliopatiwa wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni. Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake. Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray  C yamegharamiwa na Rais. Pichani, akiwa na Rais Kikwete baada ya kuwasili Ikulu .
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C, Mama mzazi RayC Margareth Mtweve (kushoto) na  dada wa Ray C Sarah Mtweve (kulia)- Picha na Freddy Maro

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages