Breaking News

Your Ad Spot

Dec 8, 2012

MAMA SALMA KIKWETE AWAANDALIA 'MENU' WATOTO YATIMA

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,(WAMA,) akiwapungia mkono watoto yatima (hawapo pichani) walihudhuria sherehe ya mwisho wa mwaka iliyofanyika kwenye viwanja vya Taasisi hiyo karibu na Ikulu jijini Dar tarehe 8.12.2012.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na mtoto mlemavu wa ngozi aliyekuwa miongoni mwa watoto yatima walioalikwa kwenye sherehe ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na taasisi yake kwa kushirikiana na Kampuni ya Saruji ya Twiga na Dar North Rotary Club kutoka vituo vya Malaika Orphan Centre (Mkuranga), Mwandaliwa Islamic Orphan Centre (Boko), Umra Orphan Centre (Magomeni), Kurasini National Orphan Centre na Mama Lenga (Kigogo).
 Mke wa Rais na Mweyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga Bwana Pascal Lesoinne kugawa zawadi mbalimbali kwa watoto yatima wanaolelewa katika baadhi ya vituo vya Dar es Salaam katika sherehe iliyofanyika kwenye ofisi za WAMA tarehe 8.12.2012.
 Baadhi ya watoto yatima wakipata chakula cha mchana walichoandaliwa na Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Twiga Cement Bwana Pascal Lesoinne mara baada ya sherehe ya mwisho wa mwaka waliyowaandalia watoto yatima kwenye ofisi za WAMA tarehe 8.12.2012.PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages