Breaking News

Your Ad Spot

Dec 3, 2012

TBL WALIPOADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI


 Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Walioathirika kwa Ukimwi cha Tocha +, Saad Ramadhan (kulia) na Arnold Goha wakiwasha mshumaa na Mratibu Mkuu wa Kifua Kikuu na Ukimwi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Hakimu Mwaikasu, wakati wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ikiadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TBL, Keneth Wanyoto. Zaidi ya watu 400 walipima Virusi vya Ukimwi siku hiyo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
 Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Walioathirika kwa Ukimwi cha Tocha +, Saad Ramadhan (kulia) na Arnold Goha pamoja na Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Orio wakiwasha mishumaa wakati wa maadhimisho hayo
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwasha mishumaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, Dar es Salaam
Banda lililowekwa na TBL  katika Soko la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam ili wafanyabiashara washiriki kupimwa virusi vya Ukimwi
 Mkazi wa Ilala Mchikichini, Abdalah Lukali (58), kushoto, akichukuliwa damu na Mshauri Nasaha kutoka Amref, tayari kupimwa virusi vya Ukimwi katika banda lililowekwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Soko la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.
 Fundi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Shabani Kilango (kushoto) akichukuliwa damu na Mshauri Nasaha kutoka Amref, Elizabeth Sangu  tayari kupimwa virusi vya Ukimwi wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiadhimisha ya Siku ya Ukimwi Duniani, Dar es Salaam juzi.
 Mtalaamu wa upishi wa TBL, Edward Mvula akichukuliwa damu tayari kupimwa virusi vya Ukimwi
Wafanyakazi wa TBL, wakinunua keki ambazo makusanyo yake walipatiwa watoto wanaoishi na virusi vya Ukimwi wa Kituo cha Tocha+
Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo (kulia) akiwauziwa keki hizo viongozi wa kampuni hiyo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin

 Mratibu Mkuu wa Kifua Kikuu na Ukimwi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Hakimu Mwaikasu, akiwasha mshumaa ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa maadhimisho hayo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TBL, Keneth Wanyoto.

Wasanii wa Tocha+ wakilia kwa uchungu walipokuwa wakiigiza igizo la UKIMWI na kugundua wote wameambukiwa kwa kutembea na Baba mwenye nyumba.Ktutoka kushoto ni Ruth Ngwembele, Gift Andrew na Emma Julius.
 Wasanii wa Kikundi cha Tocha+Fadhili Malidodi (kushoto) na Richard Kessy wakilia wakati wakiigiza igizo la UKIMWI wakati wa maadhimisho hayo.
 Dk. Mwaikasu (wa pili kushoto) akimkabidhi  Henry Ramadhan vyombo vya muziki baada ya kuwa mmoja wa washindi wa droo iliyochezeshwa kwa waliopima virusi siku hiyo.
Leonald Mitoris (kulia)wa Idara ya Uhandisi TBL, AKIPATIWA ZAWADI YA JIKO LA GESI
Meneja wa Kiwanda cha TBL, Dar es Salaam, Calvin Martine akimpatia zawadi ya jiko la gesi Josephat Magesa ambaye alikuwa miongoni mwa washindi waliopima virusu vya ukimwi

 Yolanda Minja (kulia) akipata zawadi ya jiko la gesi
 Julius Matola (kulia) wa Idara ya Mauzo wa TBL, akipatiwa zawadi ya simu
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo akimpatia zawadi ya simu Abubakar Mambo
Timu ya TBL iliyoandaa maadhimisho hayo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages