Breaking News

Your Ad Spot

Dec 1, 2012

UJUMBE WA BODI YA KIMATAIFA YA PLAN INTERNATIONAL WATEMBELEA MIRADI YA SHIRIKA HILO IKIWEMO KITUO CHA WATOTO CHA MLEGELE, KISARAWE.


Wakazi wa Wilaya ya Kisarawe wakicheza ngoma ya kiutamaduni pamoja na mmoja wa wajumbe wa bodi ya Plan International waliotembelea moja ya miradi inayofadhiliwa na shirika hilo wilayani humo.

Mlezi wa Kituo cha Mlegele Wilayani Kisarawe na Mwenyekiti wa Majengo yote ya Kulelea watoto hao Bw. Shabani Daruweshi akisoma risala kwa ujumbe wa Bodi ya Plan International (haupo pichani) ambapo amesema Shirika la Plan International limeshirikiana kikamilifu na Wanajamii, Serikali na Mashirika mengine katika kufadhili taratibu zote za kuwajengea uwezo wa kitaalam wadau mbalimbali, akitolea mfano kuijengea uwezo wa kitaalam timu ya Wilaya ya wataalam wa malezi na makuzi ya mtoto katika wilaya ya Kisarawe.
Amesema pamoja na mafanikio waliyoyapata bado wankabiliana na changamoto kadhaa ikiwemo Miundo Mbinu ya kituo kutokuwa rafiki wa watoto ikiwa ni pamoja na majengo ya kudumu, uhaba wa maji safi na salama, upungufu wa vyumba vinne vya madarasa kwa ajili ya shule ya msingi, nyumba ya walimu, ofisi, kituo cha afya ili kupunguza umbali wakupata elimu ya msingi kwa wakazi wa Mlegele.

Mlezi wa Kituo cha Mlegele Wilayani Kisarawe na Mwenyekiti wa Majengo yote ya Kulelea watoto hao Bw. Shabani Daruweshi akikabidhi risala kwa ujumbe wa bodi ya kimataifa ya Plan International ambao umesheheni changamoto kadhaa zinazohitaji kutatuliwa.

Ujumbe wa Bodi ya Kimataifa ya Plan International uliotembelea Kituo cha watoto cha Mlegele kilichopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Baadhi ya Wakazi wa Kisarawe mkoani Pwani wakisiliza yaliyokuwa yakizungumzwa na Ujumbe wa Kimataifa kutoka Plan International.

Mkufunzi wa Wauguzi Bi. Maseif Mchachura akitoa chanjo kwa mmoja wa watoto eneo la Mlegele Wilayani Kisarawe wakati Ujumbe wa bodi ya Plan International ulipotembelea eneo hilo na kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika hilo.

Gari la kutoa huduma za mbalimbali za tiba lililotolewa na Daichi Sankyo kupitia shirika la Plan International linalotoa huduma kwa jamii ya Wakazi wa Mlegele wanaoishi wilayani Kisarawe mkoani Pwani ambapo huzunguka kuwasaidia watoto wachanga wanaozaliwa hadi wamama wajawazito na wengineo.
Mfanyakazi wa Plan International kutoka nchini Kenya Grace Ndungu akichukua maelezo kutoka kwa Mkufunzi wa Wauguzi Bi. Maseif Mchachura annayetoa huduma katika Mobile Clinic iliyopo Wilayani Kisarawe kwa niaba ya Plan International.

Mkufunzi wa Wauguzi Bi. Maseif Mchachura wa Mlegele Wilayani Kisarawe akionyesha ujumbe wa Bodi ya Plan International dawa wanazotumia kusaidia kinamama pamoja na watoto wanaogua hata watu wazima wanaopata Malaria na magonjwa mengineo.

Ujumbe wa Bodi ya Plan International ukizungumza na watoto wa shule ya awali ya kituo cha Watoto cha Mlegele ambacho kimedhaminiwa na shirika hilo kuhakikisha watoto wenye umri wa kuanza shule wanaweza kupata elimu hiyo.
Mmoja wa watoto wa shule ya Awali ya Mlegele akipata kikombe cha uji.

Mmoja wa wafanyakazi wa Plan International Tanzania akionyesha jiko linalotumiwa kupika uji kwa ajili ya watoto wa shule hiyo ya awali kwa ujumbe wa bodi ya Plan International iliyotembelea kituoni hapo kukagua miradi inayofadhiliwa na Plan International.

Kichanja cha kuanikia vyombo vinavyotumiwa na watoto wa kituo cha Mlegele kunywea uji.
Baadhi ya watoto wa shule ya msingi katika kituo cha watoto cha Mlegele wakati wa ziara ya ujumbe wa bodi ya Plan International ulifika Kisarawe kukagua miradi ya Shirika hilo.
Shirika la utoaji msaada kwa watoto, Plan International (Plan), limetumia zaidi ya dola za Kimarekani milioni 100 katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili.
Plan imekuwa ikifanya kazi Tanzania kwa zaidi ya miaka 20 sasa kwa kusaidia watoto walio katika mazingira magumu na jamii ya watu masikini ili kuweza kupata huduma za afya, elimu, maji safi na salama. Hadi sasa takriban watu milioni 1.6 wamefaidika kutokana na programu hiyo.
“Kujihusisha kwa watoto katika VSLA inasaidia kuwafanya kuwa na utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwao watoto na vijana kwa kujifunza menejimenti ya fedha katika hatua za awali za maisha yao”, alisema.
Plan pia imekuwa ikisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza sera za kupinga matukio ya unyanyasaji wa watoto hasa mimba za utotoni na ajira kwa watoto. Hii imesababisha kupunguza kesi za ukatili wa kijinsia kwa watoto, amesema Chapman.
Plan inapigia debe utaratibu wa kujifunza kwa watoto kabla ya kuanza shule unaojulikana kama Maandalizi ya watoto na Maendeleo wenye lengo la kuwaandaa kuwapa msingi imara wa kielimu ili kuweza kujiunga shule.
KUHUSU SHIRIKA LA PLAN.
-Plan ni miongoni mwa mashirika kongwe na kubwa la maendeleo ya watoto Duniani. Ilianzishwa zaidi ya miaka 75 iliyopita.
-Plan inafanya kazi katika nchi zinazoendelea 50 barani Afrika, Asia na Amerika kwa lengo la kulinda haki za watoto na kuwaondoa mamilioni ya watoto kwenye umasikini.
-Plan ilianza kufanya kazi Tanzania mwaka 1991. Inafanya kazi katika wilaya saba zilizo katika mikoa mitano na wilaya zake kwenye mabano ambazo ni Dar es Salaam (Ilala), Pwani (Kisarawe na Kibaha), Mwanza (Ilemela na Nyamagana) na Geita (Geita na Nyang’hwale), na kuwafikia takriban watoto milioni 1.6.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages