Breaking News

Your Ad Spot

Jan 12, 2013

DC MAGU AFUNGA MAFUNZO YA UFUGAJI BORA KATA ZA NYIGOGO NA KAHANGARA

 MKUU wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana akizungumza jana (11.1.2013) na wafugaji wa kata za Nyigogo na Kahangara wakati wa kufunga mafunzo ya ufugaji bora yaliyoendeshwa kwa ushirikiano na Halmashauri ya Wilaya ya Magu na Kiwanda cha Kusindika Nyama cha Alpha Choice LTD, kilichopo katika kijiji cha Bugabu, wilayani humo. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Naomi Nnko na kushoto ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo wa halmashauri hiyo, Dk. Kiraba Msoke. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Naomi Nnko, akizungumza jana (11.1.2013) na washiriki wa mafunzo ya ufugaji bora kutoka kata za Nyigogo na Kahangara yaliyofanyika katika kijiji cha Bugabu, wilayani humo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana na kulia ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo katika halmashauri hiyo, Dk. Kiraba Msoke. Mafunzo hayo yaliyoanza Januari 9, mwaka huu na kumalizika jana yaliandaliwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu na Kiwanda cha Kusindika Nyama (Picha zote na Emmanuel Ndege)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages