Breaking News

Your Ad Spot

Jan 13, 2013

LORI LAUA WANNE NA KUJERUHI 29, SIMIYU, BAADA YA KUPINDUKA LIKIENDA MNADANI

SIMIYU, Tanzania
Watu wanne wamekufa papohapo na wengine 29 kujeruhiwa baada ya  lori aina ya Fuso kupinduka katika kijiji cha Lugulu wilaya ya Itimila mkoani Simiyu.
    Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu,  Salum Msangi, alisema kuwa ajali ajali hiyo imehusisha Lori lenye namba T173 na imetokea leo muda wa saa moja asubuhi, likitokea Bariadi mjini kwenda Mwamapalala mnadani likiwa na abiria mizigo.
   Alisema likiwa katika mwendo kasi liliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo, majeruhi na mali kadhaa kuharibika.
   Alisema kuwa watu aliokufa bado hawajatambulika majina yao, huku akiongeza kuwa watatu ni wanawake na mmoja  mwanaume.
Kamanda huyo alieleza  majeruhi katika ajali hiyo, 8 ni wanawake 21 wanaume amabapo walikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya bariadi kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
   Alieleza kuwa dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Musa, na baada ya ajali hiyo dereva huyo aliweza kutoroka na hadi sasa anatafutwa na jeshi la polisi kuweza kumfiikisha mahakani kujibu tuhuma.
    Aliwataka madereva wa magari yanayobeba mizigo ya minadani kutochanganya mizigo na abiria, na kufanya hivyo ni kosa la usalama barabarani.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages