Breaking News

Your Ad Spot

Jan 27, 2013

MSAFARA WA KINANA KWA TRENI KUTOKA DAR WAWASILI KIGOMA SALAMA LEO ASUBUHI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake, wakikaribishwa na viongozi wa CCM mkoa wa Kigoma baada ya treni kutoka Dar es Salaam, kuwasili leo asubuhi mjini Kigoma, Wanaoshuka ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi NapeNnauye. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose  Migiro (kushoto) wakisindikizwa baada ya kushuka kwenye treni mjini Kigoma, ambako waliwasili leo wasubuhi wakitoka jijini Dar es Salaam.Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
 Mamia ya wananchi wakiwa wamejitokeza kupokea msafara wa Kinana ulipowasili kwa treni Stesheni ya Kigoma leo asubuhi. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokewa kwa ngoma kwenye stesheni ya Kigoma, alipaowasili kwenye stesheni hiyo na ujumbe wake akitokea jijini Dar es Salaam. Wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Walid Kaborou na kulia ni Nape akishiriki kupiga ngoma. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshukuru dereva wa treni Kambi Ali, baada ya treni ya abiria aliyoendesha akiwemo Kinana na ujumbe wake kuwasili mjini Kigoma leo asubuhi. Wengine Wapili kushoto ni Dk. Asha Rose Migiro na Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akimfurahia mtoto Ali Saidi mwenye umri wa miezi minane, ambaye ni mtoto wa  mmoja wa abiria aliowakuta kwenye  Stesheni ya Kigoma, msafara wa Kinana ulipowasili leo kwa treni.Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
 Abiria wakiwa katika behewa la daraja la watatu, wakitoka Tabora kwenda Kigoma leo
 Mwananchi wa Kaliua akipeleka kupakia mchele kwenye behewa, treni ilipofika stesheni ya eneo hilo mkoani Kigoma leo.
 Kula kila dalili kwamba safari za treni zinachochea baadhi ya biashara kufanyika hasa maeneo ya vijiji vyenye stesheni. Pichani wananchi wakiuza miwa kwenye stesheni ya Kazuramimba mkoaniu Kigoma, leo treni ilipopita ikienda  mjini Kigoma
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwasilimia wananchi kwenye stesheni ya Urambo mkoani Tabora
 Wadau waliosafiri katika treni yenye msafara wa Kinana na ujumbe wake, wakiwa katika treni hiyo kabla ya kufika Kigoma
 Kila mmoja kwa raha zake kama huyu jamaa
Msichana akiwa na miwa kwenye stesheni ya Kazuramimba ambako ni maarufu kwa uuzaji wa viburudisho hivyo (Picha zote na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages