Breaking News

Your Ad Spot

Jan 23, 2013

WATANO WAFARIKI MAGU KWA AJALI YA HICE


MAGU, Tanzania
WATU watano wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea  wilayani Magu, mkoani Mwanza, baada ya hiace moja kuigonga kwa nyuma hiace nyingine iliyokuwa imeegeshwa nje ya pembezoni mwa barabara, na kusababisha gari hiyo kuanguka kwenye korongo la maji.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, iliyotokea jana saa12:35 jioni katika barabara kuu ya Mwanza-Musoma, eneo la kijiji cha Ikelebelo, kata ya Kahangara, wilayani Magu na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.

Alisema kuwa baada ya hiace kugonga kwa nyuma hiace nyinge, ilikosa mwelekeo na kuanguka kwenye korongo la maji.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya ya Magu, Mkuu wa wilaya hiyo, Jacqueline Liana, amewataja watu waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Ramadhan Bulemela (25), mkazi wa Magu, Beatrice Lenatus (21), mkazi wa mwanza, Ruhumbika Manyama (22), mkazi wa Mwanza, na dereva wa gari hiyo Kevin Peter ambaye amefariki akiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando.

Jacqueline alisema kuwa mwanaume mmoja aliyekufa kutokana na ajali hiyo bado jina lake halijafahamika na kwamba mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya mjini Magu.

Alisema kuwa ajali hiyo iliihusisha hiace moja yenye namba za usajili T.180 BLS, Iliyokuwa ikitoka mjini Magu ikielekea Buzuruga jijini Mwanza, ambapo iliigonga kwa nyuma hiace yenye namba za usajili T.770 BMK, iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara hiyo.

Mganga mkuu wa wilaya ya Magu, Dk. Athuman Pembe, alisema kuwa katika ajali hiyo watu watatu walikufa papo hapo, mmoja akafariki akiwa katika hospitali wilaya ya Magu na dereva wa hiace hiyo akafariki akiwa katika hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza.

Dk. Pembe alisema kuwa walipokea jumla ya majeruhi 13 hospitalini hapo, ambapo baadhi yao walitibiwa na kuruhusiwa na kwamba majeruhi wengine hali zao zinaendelea vizuri.

Alisema kuwa majeruhi wengine ambao bado wako hospitalini hapo ni pamoja na Libia Lebeli (18), mkazi wa National Magu, Masalu Ezekiel (23), mkazi wa Nyanguge Magu, Catheline Mathias (30) na Paul Mahaboalila (17) mkazi wa Mwanza.

Aliwataja majeruhi wengine kuwa ni pamoja na Neema Mathias (20) mkazi wa Hilula, Magu, Pendo Benard (28) mkazi wa Kipeja Magu, Mwinyi Daud (28), mkazi wa mtaa wa benki mjini Magu, Joseph Edward (20), na Hamisi Yashikaga, wakazi wa Isandula Magu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages