Kinana akikagua athari za vurugu za gesi Mtwara |
MTWARA, Tanzania
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Abdulrehaman Kinana amewataka wananchi mkoani Mtwara kuwa watulivu na mshikamano katika kipindi hiki cha kutafakari maafa yaliyotokea na kuona hayatokei tena.
Rai hiyo aliitoa leo mjini Masasi alipowatembea watu na maeneo yaliyoathiriwa na vurugu zilizojitokeza mwishoni mwa mwezi uliopita za madai za kupinga mradi mkubwa wenye manufaa kwa mikoa hii na taifa kijumla wa bomba la gesi.
Aliwaambia wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya hiyo pamoja na wananchi katika maeneo ya matukio kuwa hiki ni kipindi cha kuwa watulivu na mshikamano uliyokuwepo ili mkurejesha amani iliyokuwa hatarini kutoweka.
Katika fujo hizo zilizojitokeza katika wilaya tatu za Mtwara Newala na Masasi ambayo ndiyo iliyoathiriwa vibaya kwa kuuwawa watu wanne na wengi wengi walijeruhiwa.
Wilaya hiyo majengo 17 yakiwemo ofisi za serikali, mahakama,vituo vya polisi, nyumba za wabunge, polisi na ofisi za CCM wilaya na kata pamoja na magari yalichomwa moto na kuteketezwa kabisa.
Katibu Mkuu alisema maafa yaliyotekea ni makubwa na alifanya ziara hiyo ya haraka jana kwa ajili ya kuja kuwafariji kwa kuwapa pole wale wote waliyofikwa na madhara hayo pamoja na wananchi kijumla katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Alisema waliyofanya vitendo hivyo ni wahalifu wabaya ambao vyombo vya dola vinatawachukulia hatua za kisheria.
Katibu Mkuu ambaye alifuatana na katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa siasa na Ushirikiano wa mambo ya nje Asha Rose Migiro alisema Chama kitaangalia namna gani watashirikiana na wilaya zilizoathiriwa katika kujenga majengo yake.
Alisema kwa kuanzia anatuma shs laki tisa za matengenezo ya gari la Chama wilaya ya Masasi lililohabiriwa ili waweze kupata usafiri.
Alisema ana imani na hotuba ya Rais iliyojikita katika maelezo ya hoja za miradi ya gesi na maendeleo ya mikoa ya Mtwara na Lindi imeeleweka kwa wananchi na kwamba hakuna sababu tena ya viongozi kurudia rudia.
Katibu Mkuu aliwaasa wananchi kutumia njia zinazofaa katika kujenga hoja kwa matatizo au mambo yasiyoeleweka na katika kutatua kero mbali mbali.
Alikamilisha ziara yake leo jioni kwa kutembelea maeneo ya majengo yaliyoathiriwa Mtwara mjini pamoja na kuzungumza na kamati ya siasa ya Mtwara mjini na Vijijin.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269