MBEYA,Tanzanaia
POLISI wa kituo cha Mkwajuni, wilayani Chunya Jafari Mohamed (30)na jambazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Shabani Msule, wamekufa katika mpambano wa kurushiana risasi, lilotokea usiku wa kuamkia leo, mkoani Mbeya.
Akithibitisha tukio hilo, Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki, alisema tukio hilo limetokea saa 7:30 usiku wa kuamkia leo, na kwamba Mohamed alifariki dunia katika hospitali ya Mwambani iliyopo Mkwajuni wilayani humo, wakati akiendelea kutibiwa jeraha hilo la risasi kwenye ubavu wake wa kulia.
Alisema majambazi wanne yakiwa na silaha inayodhaniwa kuwa ni aina ya SMG yalivamia kituo cha mafuta mali ya Samora Muyombe, kilichopo kijiji cha Matundasi, ambako inadaiwa walipora sh. milioni 2.2.
Kamanda alisemaa kuwa majambazi hayo yalikuwa yakitumia gari namba T.227 BST aina ya Toyota Corola lililokuwa likiendeshwa na marehemu Shaban Msule (33), mkazi wa Makambako.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda Masaki, marehemu PC Mohamed akiwa doria na askari wenzake walifuatilia tukio hilo na katika mapambano ya kurushiana risasi ndipo alipojeruhiwa kwa kupigwa risasi ubavu wa kulia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269