Breaking News

Your Ad Spot

Feb 20, 2013

MAMA SALMA JK AMALIZA ZIARA LINDI

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, wilaya ya Lindi mjini, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikagua mtaro katika mtaa wa Wailes Lindi mjini, leo. Mtaro huo unadaiwa kusababisha maafa ya mafuriko kuua watoto watano mwaka jana, kutokana na kumwaga maji mitaani wakati wa mvua badala ya kufuata mkondo wa mtaro. Mama Salma amewapa pole waliopoteza watoto wao na kuagiza Halmashauri ya wilaya hiyo kusimamia ili mtaro huo ujengwe kwa kiwango kinachotakiwa.
Vijana wakila kiapo baada ya kukabishiwa kadi zao za UVCCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mama Salma Kikwete kwenye mkutano uliofanyika Kata ya Waile Lindi mjini.
Mzee Ismail Bakari (80) maarufu kwa jina la Kulombandila akimuuliza swali mama Salma Kikwete kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Ofisi ya CCM, wilaya ya Lindi mjini leo.
Kina mama wa Kata ya Mikumbi Lindi wakimpa zawadi ya mkeka Mama Salma Kikwete kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye kata hiyo.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Kata ya Kikumbi 
Hashim Masoud kutoka CUF akikabishi kadi yake kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete baada ya kaumua kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mikumbi, leo. Wanachama 25 wakiwemo watano kutoka CUF walijiunga CCM

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages