Breaking News

Your Ad Spot

Feb 24, 2013

MAONYESHO YA SHANGAA-ART OF TANZANIA YATIA FORA JIJINI NEW YORK

Queense Community Collage ambacho ni sehemu ya mtandao wa Vyuo vikuu vya Jiji la New   York  ( City University of New York )  mwishoni wa wiki kiliandaa maonesho   sanaa za kitanzania. Maonesho    hayo  yaliyofanyika katika Chuo hicho  yanaelezwa na   waandaji  ni ya kwanza kufanyika nje ya Tanzania na Ujerumani,  yalipewa  jina  la  SHANGAA-Art of Tanzania likihusisha mkusanyiko  sanaa zaidi ya  112 lakini  kila moja ikibeba maudhui yake. Kwa kweli kama lilivyo  jina la maonesho hayo, ziliwashagaza wageni mbalimbali waliohudhuria maonesho hayo.  Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (pichani akifungua maonyesho hayo), ndiye aliyepamba maonesho hayo  kama mgeni wa heshima, akiambatana  na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania Nchi Marekani, Bi. Lily Munanka.  Sanaa zilizopamba maonyesho hayo  zilikuwa ni za kuchonga nyingi kati yake zikitoka katika Mikoa ya  Usukumani na Umakondeni. Laini pia kulikuwa na video zilizokuwa zikionyesha aina mbalimbali za ngoma zikionyesha mila na utamaduni wa mtanzania katika uhalisia wake.  Jumla ya  sanaa 121 zilikusanywa kutoka wa wadau mbalimbali lakini ni 112 tu zilizoweza kuoneshwa kutokana na uhaba wa nafasi. Kwa kutambua umuhimu wa maonyesho hayo  Halmashauri ya Jiji la New York ilitoa Hati kwa waandaaji wa maonesho hayo.   






No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages