Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipeana mkono na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulembe wakati ujumbe kutoka shirika hilo ulipofika ofisini kwake kuandikisha viongozi wa Serikali katika Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF mjini Zanzibar leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akijaza fomu ya uanachama wa Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhusu Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiweka saini ya dole gumba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ofisini Kwake Vuga mjini Zanzibar baada ya kujiunga na NSSF. Kushoto ni Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Dodoma, Mariam Ahmed, Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu na Ofisa Uendeshaji NSSF, Ally Mkulemba.
Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akimkaribisha ofisini kwake Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed alipofika kwa ajili ya Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akifafanua jambo kuhusu Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo. Kulia ni Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akiweka saini ya dole gumba.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Said Shaaban Said.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Said Shaaban Said.
Na Mauwa
Mohammed, Zanzibar
MAKAMO
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Mfuko wa Taifa
wa Hifadhi ya Jamii Tanzania (NSSF) utafanya utaratibu
wa kuishawishi mifuko mengine ya Jamii kuanzisha miradi ya Jamii ili
kuongeza pato la wanachama pamoja na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Kauli
hio alitoa wakati akijaza
fomu maalum ya kuomba kujikunga kuwa mwanachama rasmi wa Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii { NSSF } hafla
iliofanika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
Alisema
mfuko huo umeonyesha mwanga na matumaini makubwa kwa wanachama wake hasa
kutokana na miradi mingi iliyoianzisha ambayo kwa Asilimia kubwa inalenga
kuwanufaisha wanachama wake hasa wale wenye kipato cha chini.
Balozi
Iddi alisema NSSF ni chombo cha wananchi kwa vile kinajihusisha moja kwa moja
na hatma ya washirika wake ambao wengi wao ni wafanyakazi wenye kipato cha
chini.
Aliuahidi
Uongozi wa Mfuko huo wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwamba amehamasika ya mfumo
wa mfuko huo na kupelekea moja kwa moja kuamua kujiunga ambapo ameahidi
kuchangia kila baada ya kipindi cha miezi mitatu.
Mapema
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii { NSSF } Mkoa wa Dodoma ambao ndio uliopewa
jukumu la kuhudumia Viongozi wa ngazi ya Juu Bibi Maryma Ahmed alisema
zaidi ya Wabunge 165 wamekubali kujiunga kwa hiari kuwa wanachama wa Mfuko huo.
Bibi
Maryam alimueleza Balozi Seif kwamba wabunge hao hupatiwa mafao yao mara
wamalizapo utumishi wao wa Bunge sambamba na huduma za matibabu wakati wa
kipindi chote cha kazi zao.
Hata
hivyo Meneja huyo wa NSSF Kanda ya Dodoma alieleza kuwa wapo Wabunge wastaafu
waliomaliza wadhifa wao lakini bado wanaendelea kuchangia mfuko huo kwa vile
bado wana fursa iliyo wazi ya kufanya hivyo.
Nae waziri katika
afisi ya Makamom wa pili wa rais Mohamme Aboud Mohammed amesema wananchi wa
Zanzibar bado hawajapata mwamko mzuri wa kujiunga na mfuko wa hifadhi ya
jamii NSSF.
Alisema wananchi wengi watakuwa tayari kujiunga
na mfuko huo endapo wataelimishwa juu ya faida watakozipata kwa kujiunga na
mfuko huo.
Alisema ni vyema wakulima wa karafuu ,
wavuvi na wajasiri amali wadogo wadogo kuelimishwa ili wapate kujiuna na mfumo
huo kwa lengo la kuwasaidia.
Meneja wa
NSSF Mariyam Mohammed alisema wajasiri amali
wadogo wadogo na sekta zisizo rami watafaidika endapo
watajiunga na mfuko huo wa hiari ambao
utasaidia maisha yao ya baadae.
Alisema wafanyikazi wa
sekta zisizo rasmi kabla haujanzishwa
mfuko huo wa hiri walikuwa hawachukuliwi na sekta nyengine yeyote isipokuwa
yule aliyeajiriwa katika sekta binafsi tu.
Hivyo mfuko huo wanachama
wake wataweza kupata mafao yao saba yakiwemo ya kumia kazini,msaada wa uzazi
kwa mama waja wazito,msaada wa mazishi , pamoja na mfuko wa afya.
“Kina mama waja wazito watafaidika
na mafao
ya mfuko wa hiari endapo watajiunga na
mfuko huo”alisema Bi Maryam .
Mafao mengine yatakuwa ni baada ya muda
miaka mitatu kuchangia mfuko
huo ni
mafao ya pensheni ya ulemavu , pensheni urithi
na pensheni
ya uzee .
Alisema wanachama wengi wasio rasmi
wanapata shida ya matibabu kwa vile hawana kiasi rasmi cha fedha ambazo
wataweza kujitibia hivyo kujiuna na mfumo huo wa hiyari watapata matibabu ya
bure endapo watapata matatizo ya kiafya pamoja na
familia zao.
Balozi
Seif amesajiliwa kuwa mwanachama wa Mfuko huo wa Taifa Hifadhi ya Jamii baada
ya kukamilisha taratibu zote za kujaza fomu ya usajili mbele ya Timu ya Maafisa
wa mfuko huo ikiwemo pia kupigwa picha kwa ajili ya kupatiwa kitambulisho rasmi
cha uwanachama kamili wa mfuko huo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269