Breaking News

Your Ad Spot

Mar 7, 2013

MWILI WA MAREHEMU RAIS HUO CHAVEZ WA VENEZUELA WAAGWA



Mwili wa mareheu rais Hugo Chavez wa Venezuela, umelazwa katika kituo cha mafunzo ya jeshi katika mji mkuu Caracas
Mapema leo mwili wa marehemu Chavez ulipitishwa kwenye umati mkubwa wa wafuasi wake katika mitaa ya mji mkuu Caracas.
Taarifa zinazohusiana
Siasa
Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .
Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa heshma zao .
Makamu wa rais Nicolas Maduro anaongoza shughuli hiyo.
Mwili wa rais Chavez umepelekwa katika chuo cha kitaifa cha mafunzo ya kijeshi ambapo utazikwa kesho Ijumaa.
Bwana Chavez alifariki akiwa umri wa miaka 58 baada ya kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili.
Maelfu ya watu awali walikwenda barabarani mjini Caracas kutoa heshima zao za mwisho kwa Chavez wakifuatana na gari lililokuwa limebeba jeneza lake kuelekea katika chuo cha mafuzno ya jeshi.
Mazishi ya kitaifa ya Chavez yatafanyika Ijumaa.
Mkuu wa ulinzi wa Rais alinukuliwa akisema kuwa alikuwa na bwana Chavez alipofariki.
Generali Jose Ornella, alisema kuwa Chavez alifariki kutokana na mshtuko wa moyo na katika siku zake za mwisho kabla ya kifo cha ealisema angependa kuendelea kuishi.
Jeneza lake lililokuwa limefunikwa bendera ya nchi hiyo uliwekwa katika ukumbi ambao ni kumbukumbu ya waliopigania uhuru wa watu wa Amerika ya Kusini
Maelfu ya watu walipanga foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Chavez, wakiwemo maafisa wa serikali na viongozi wa Amerika ya Kusini,kama Rais wa Bolivia Evo Morales na Rais wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner. KUTOKA BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages