Breaking News

Your Ad Spot

Apr 10, 2013

LOWASSA AWAMWAGIA MAMILIONI WAISLAM

Waziri Mkuu wa zamani, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akikabidhi kitita cha sh. milioni tano kwa viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa BAMITA, Sheikh Salum Sung'he. Imeelezwa katika makabidhiano hayo kwamba fedha hizo ni kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi ya BAMITA katika kuelimisha jamii katika kupunguza maambukizi ya Ukimwi na kudhibiti mimba kabla ya ndoa. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa BAMITA, Alhaj Juma Swalehe.  Huu ni mwendelezo wa Lowassa kumwaga mamilioni ya fedha kwa taasisi za dini ambapo amewahi pia kumwanga mara nyingi mamilioni ya fedha kwenye makanisa kupitia harambee mbalimbali. PICHA NA .DAILY MITIKASI BLOG

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages