DODOMA, Tanzania
MREMBO wa Tanzania wa mwaka 2012, Brigitte Alfred, leo amedhihirisha kuwa Utanzania wake una walakini baada kushindwa kuzungumza Lugha ya Taifa ya Kiswahili kwenye semina mjini Dodoma.
Kufuatia kituko hicho, Mrembo huyo (pichani), alitingwa na wakati mgumu baada ya wabunge kumtaka kuzungumza kiswahili lakini yeye akisisitiza asizungumze lugha hiyo eti haijui vizuri kama anavyojua lugha ya kigeni ya Kiingereza..
Brigitte alifikwa na aibu hiyo aliposimama kutoa mada katika semina ya wabunge kuhusu kuwajengea uelewa kuhusu watu wa jamii ya albino ambapo mara baada ya kusimama alianza kuzungumza lugha ya kiingereza.
Hata kabala ya kumaliza sentesi moja katika utangulizi wa hotuba yake wabunge walianza kuguna mfululizo hivyo kumfanya anyamaze na kuamua kujitetea na kuomba msamaha aruhusiwe aendelee kutumia Kiingereza eti kwa kuwa kiswahili chake siyo kizuri hivyo hivyo anahofia kichekwa.
"Waheshimiwa naomba mniruhusu niendelee na kiingere za kwani Katika umri wangu muda mwingi nimeishi Kenya hivyo siwezi kiswahili sawa sawa," alisema mrembo huyo hatua iliyofuatiwa na Mwenyekiti wa semina hiyo Magnet Sitka kuwaomba wabunge kumsamehe
Katika some lake Brigitte aliwaomba wabunge kumuunga mkono Katrina jitihada zake katika kuwatetea albino.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269