Breaking News

Your Ad Spot

Apr 14, 2013

KINANA AANZA ZIARA YA KIKAZI MOROGORO


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Innocent Edward, wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika eneo la Nane Nane, nje kidogo ya mji wa Morogoro, leo. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro mjini Fikiri Juma. Kinana amewasili mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya siku nane kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa ilani ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili eneo la Nane Nane mkoani Morogoro kuanza ziara ya siku nane ya kikazi mkoani humo, leo Aprili 14, 2013.
 .Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi baada ya kuwasili Ofisi Kuu ya CCM mkoa wa Morogoro, leo Aprili 14, 2013. Kinana amewasili Morogoro kwa akili ya kukagua uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.(Picha na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages