Breaking News

Your Ad Spot

Apr 26, 2013

RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MUUNGANO

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiingia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tayari kuwaongoza maelfu ya watu waliohudhuria kilele cha sherehe za Miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika leo.
 Amiri Jeshi mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa gwaride rasmi lilioandaliwa katika kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe zilizofanyika leo asubuhi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru jiji Dar es Salaam kuhudhuria maadhimisho ya Sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa kilele cha Sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo asubuhi (picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages