Breaking News

Your Ad Spot

Apr 9, 2013

UHURU KENYATTA AAPISHWA LEO KUWA RAIS WA AWAMU YA NNE WA KENYA

Rais Uhuru Kenyatta akipunga mkono baada ya kuapishwa
NAIROBI, Kenya.
  SHAMRASHAMRA, nderemo na vifijo vimehanikizwa leo wakati wa shereheza za kuapishwa wa Rais wa nne wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
      Sherehe za kuapishwa kwa kiongozi huyo zilmefanyika kwenye uwanja wa Kasarani – Moi huku zikiwa zimeweka rekodi ya kuhudhuriwa na watu wengi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 70,000.
      Licha ya haamasa, kuwepo miongoni mwa wananchi tangu walipoingia uwanjani asubuhi, hamasa hiyo ilizidi Kenyatta na Ruto walipokuwa wakiapishwa.
      Sherehe hizo za kuapishwa kwa Kenyatta na Naibu Rais William Ruto, zilihudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais Jakaya Kikwete ambaye wakati wa kuingia uwanjani alishangiliwa sana kama ilivyokuwa kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Paul Kagame wa Rwanda na Al Bashir wa Sudan.
      Viongozi wengine waliohudhuria ni marais Josepha Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Omar Bongo wa Gabon, Goodlack wa Nigeria, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Pierre Nkurunzinza. Wengine ni kutoka Sudani Kusini, Ethiopia na Somali
       Ulinzi uliimarishwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Nairobi na kwenye uwanja wa Kasarani –Moi, hadi mgeni mwalikwa anaingia ndani alikuwa anapekuliwa zaidi ya mara tano na askari na wanajeshi waliokuwa wametanda  kila kona.
     Wananchi waliofika uwanjani hapo walikuwa wakishangilia kwa kusema: “Sio nusu ni nzima,” na “Kitendawili kimeteguliwa,” huku wakishangilia kama inavyokuwa kwenye mechi kubwa za mpira wa miguu.
      Viongozi wengine wa Kenya walioshangiliwa sana mbali ya Kenyatta na Ruto ni marais wastaafu Mwai Kibaki na Daniel arap Moi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages