Breaking News

Your Ad Spot

Apr 15, 2013

UTT YAZINDUA HUDUMA MPYA YA MIKOPO KWA AJILI YA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji  (UTT), Dk. Hamis Kibola akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya
ya kukopesha kwa ajili ya kuendeleza biashara kwa wafanyabishara wadogo na wa
kati kwa masharti nafuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano, Daudi Mbaga
na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akimkabidhi mkopo wa shis milioni 4 Mkuu wa madereva wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, Mrisho Ngongo.
Picha ya pamoja

Na Mwandishi Wetu

 MFUKO wa Dhamana ya Uwekezaji (UTT) imeanzisha huduma mpya
ya kukopesha kwa ajili ya kuendeleza biashara kwa wafanyabishara wadogo na
wakati kwa masharti nafuu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mwendeshaji Mfuko huo James Washima alisema kuwa mfuko umetimiza miaka 10
ambapo imeanzisha huduma hiyo ili kuweza kukuza uchumi kwa wananchi.

Washima alisema kuwa waliowekeza katika mfuko wa uwekezaji
wa pamoja na UTT watachukua mikopo kwa kutumia vipande wanavyomiliki kama
sehemu ya dhamana na ikiwa pamoja kuondolewa kwa gharama za kujiunga.

vipande katika mfuko huo kutarahisha kukopa na kupunguza
gharama kuweza kujiunga katika uwezeshwaji wa mikopo.

Alisema kuwa waliowekeza vipande hawataweza kukopa dhamani
yote iliyowekezwa katika mfuko lengo ni kuendelea kustawisha kiuchumi kwa
wananchi na kuona umhimu wa uwekezaji katika mfuko huo.

Washima alisema lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kutoa
suluhisho kwa wajasiriamali wadogo ,mfuko wa kuweka na kukopa (SACCOS) na
mwananchi mmoja moja katika upatikanaji wa mitaji kwa  kuwezesha kutekeleza miradi ya kiuchumi.

Aidha alisema kuwa wameweka mfumo ambao utaweza kurahisisha
kuwafikia wananchi wa vijijini kuweza kukopa hata kama hawako katika mfumo wa
uwekezaji wa vipande.

Alisema mikopo hiyo katika madaraja  manne ya mtu mmoja moja,kupewa dhamana ya mtu
aliyewekeza katika mfuko huo,mkopo kwa ajili ya taasisi  pamoja na mkopo wa biashara.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages