Breaking News

Your Ad Spot

Apr 19, 2013

ZIARA YA KINANA MVOMELO, AVALIA NJUGA MGOGORO WA MTIBW SUGAR NA WAKULIMA WA MIWA, WASTAAFU

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Menejimenti ya Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa na wakulima na miwa, leo Aprili 18, 2013, wilaya ya Mvomelo mkoani Morogoro. lengo la kikao hicho ilikuwa kuzungumzia mgogoro uliopo baina ya kiwanda hicho na wakulima na wastaafu wa kiwanda hicho, kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kuhusu wakulima kucheleweshewa malipo ya miwa yao.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Wakulima wa miwa Mtibwa, Khadija Kondo akieleza matatizo mbalimbali kati ya wakulima na kiwanda cha Sukari cha Mtibwa,wakati wakulima wa miwa na wastaafu wa lipokutanishwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu matatizo mbalimbali.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungua shina la wakereketwa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), la timu ya soka ya Villa, Kata ya Midizini, Mtibwa wilayani Mvomelo mkoani Morogoro, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa chama mkoani Morogoro.

Katibu wa Shina la wakereketwa wa UVCCM, la Timu ya soka ya Villa, Kata ya Midizini, Mvomelo, Salum Mshana akisoma risala ya tawi hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipofungua shina hilo leo Aprili 19, 2013.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages