NA IMMACULATE MAKILLA, DOM
SERIKALI imemwajiri Mtaalamu Mshauri wa kusanifu miundombinu ya maji katika mji wa Magu,hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete la kutatua tatizo sugu la maji kwenye eneo hilo mji wa huo.
Naibu Waziri wa Maji Binilith Mahenge alisema hayo alipokuwa akijibu swali la Dk. Festus Limbu Mbunge wa Magu –CCM lililouliza ,je, Serikali haioni kuwa haiwatendei haki wananchi wa mji wa Magu kwa kutotekeleza ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais.
Aidha Naibu huyo alisema kuwa usanifu huo uliohuisisha miji midogo ya Magu ,Nansio,Misungwi,Ngudu,Sengerema,Geita pamoja na jiji la Mwanza,na ulikamilika mwezi Septemba mwaka 2011.
Usanifu huo uligharimu sh. bilioni 1.1 ambapo gharama ya ujenzi kwa mji wa Magu ilikadiriwa kuwa sh. bilioni 24.
Hata hivyo Serikali kwa kushirikiana na wafadhili itagharamia ujenzi wa miradi ya maji ya jiji la Mwanza ,miji ya Misungwi ,Magu ,Lamadi na usafi wa mazingira kwa miji ya Bukoba na Musoma.
Benki ya Maendeleo ya Ulaya (EB) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) watatoa jumla ya Euro milioni 105 sawa na sh. bilioni 214 kugharamia utekelezaji wa miradi hiyo.
Kabla ya kuanza ujenzi ,wafadhili waliona wajiridhisha na gharama zaujenzi kwa kufanya mapitio ya usanifu uliofanyika awali na kujumuisha vijiji vilivyopo umbali wa kilometa 12 kutoka bomba kuu.
Wataalamu washauri wanaopendekezwa kufanya mapitio ya usanifu wa miradi hiyo watawasilisha mapendekezo yao ya kiufundi na kifedha mwanzoni mwa mwezi June mwaka 2013,alisema Naibu Waziri huyo.
Your Ad Spot
May 10, 2013
Home
Unlabelled
AGIZAO LA, RAIS KIKWETE LA AHADI YA MAJI MAGU LAANZA KUTEKELEZWA
AGIZAO LA, RAIS KIKWETE LA AHADI YA MAJI MAGU LAANZA KUTEKELEZWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269