Msanii
wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Snura akiimba jukwaani
wimbo wake unaotamba kwa sasa katika vituo vingi vya redio,uitwao
Majanga,mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uwanja wa Jamuhuiri
jioni ya leo wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM ilipokuwa ikizindua
msimu wake mpya kwa wasikilizaji wake,uzinduzi huo ulikwenda sambamba na
kufanyika kwa semina ya fursa kwa Watanzania.
Aidha msimu huo umekwenda
sambamba na kaulimbiu inayofuatia harakati za MADE IN TANZANIA,ambapo
msukumo wake ni kuwashawishi Watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa
hizo kwa umoja wa maendeleo,huku neno TWENZETU likitumika kama neno
rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi uzinduzi huo utabeba harakati
rasmi za vita dhidi ya Uharamia wa kazi za wasanii,Wabunifu na wavumbuzi
mbalimbali.Kesho kutakuwepo na matembezi ya kampeni ya kupinda uharamia
wa kazi za sanii yatakayoanzia uwanja wa Jamuhuri mapema asubuhi na
kupolewa na Waziri Mkuu Mh. Pinda.
Msanii
mahiri wa Mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akiwakuna vilivyo wakazi wa
mji wa Dodoma jioni ya leo.alipowaangushia maneno kadhaa na umati
kulipukw ana mayowe kila kona,ambapo Clouds FM wamezindua msimu wao
mpya.
Maelfu
ya Watu wakiwa ndani ya uwanja wa jamuhuri jioni ya leo wakijumuika kwa
pamoja na wana Clouds FM walipokuwa wakizindua msimu wao mpya.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip
Hop,Izzo Bizziness akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi
wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda
kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya,Madee akitumbuiza mbele ya umati mkubwa wa
watu ndani ya uwanja wa jamuhuri,wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM
kilipokuwa kikizindua msimu wake mpya.
Pichani
shoto ni Mkurugenzi wa vipindi na Utafiti,Ruge Mutahaba akizungumza na
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ndani ya Uwanja wa Jamuhuri
jioni ya leo,wakati tamasha la uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM
likiendelea,Nape alifika uwanjani hapo kujionea shamrashamra mbalimbali
zilizojumuisha maelfu ya watu.
Palikuwa hapatoshi uwanja wa jamuhuri Dodoma jioni ya leo.
Msanii wa mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop,Afande Sele a.k.a Baba Tunda akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269