Breaking News

Your Ad Spot

May 7, 2013

CCM YAKASIRISHWA ULIPUAJI BOMU KANISANI ARUSHA

*YATAKA WAL IOHUSIKA WAPATIKANE NA KUPEWA ADHABU KALI YA MFANO
Ndugu Kinana
DODOMA,Tanzania
CHAMA cha Mapinduzi CCM kimelaani vikali tukio la kutupwa kwa bomu katika Uzinduzi wa kanisa la Mtakatifu Joseph Arusha na kuua watu watattu.

Mbali na hivyo imeitaka serikali kutumia vyombo vyake vyote kuhakikisha watuhumiwa wa tukio hilo wanakamatwa na kupata adhabu kali itakayo kuwa fundisho kwa wengine wenye mawazo ya kufanya hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na katibu  Mkuu wa CCM Abrahaman Kinana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini hapa.

“ Chama cha mapinduzi kimeshtushwa na tukio hilo na kimesikitishwa sana  kwani ni kitendo kisichokubalika ndani ya jamii yeti” alisema Kinana .

“Tunatoa salaam za rambirambi kwa waliofikwa na msiba na kwa wale waliojeruhiwa tunamuomba Mungu awape nafuu mapema”

Kinana alisema tukio hilo ni baya na la kiharamia na kama ni mtandao ni lazima serikali ihakikishe unauvunja kwa nguvu zote.

Alisema watanzania wote bila kujali itaikadi ni lazima kupiga vita vitendi vya aina hiyo vinavyogharimu maisha ya watanzania .

Alisema kitendo hicho akikubaliki na kitendo kipya kwa taifa la kitanzania.

“Zichukuliwe hatua kali dhidi ya wataobainika ili asitokee mwingine akajaribu kufanya hivyo tena” alisema Kinana.

“Na kama ni mtandao ni lazima kwa serikali kutumia nguvu zote kuhakikisha kuwa mtandao huo unavunjwa “ alisisitiza katibu Mkuu.

Kauli hiyo ya Katibu Mkuu imefuatia kutokea kwa mlipuko  juzi majira ya saa 4.30 asubuhi  katika kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi parokia ya Olasiti Jijini Arusha.

Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya kuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia hiyo.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa balozi wa Vatican nchini nan mjumbe wa baba Mtakatifu  Askofu  Fransisco Mantecillo padila.

Mlipuko huo ulitokea wakati mgeni huyo rasmi alipokuwa akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi wa kanisa hilo .

Wakati akiwa katika hatua hiyo mtu asiyejulikana alirusha  kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea kwenye mkusanyiko wa watu na baada ya kutua kilisababisha kishindo kikubwa na mlipuko mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages