DK. MNDOLWA |
KONDOA, Tanzania
MWENYEKITI wa Wazazi Mkoa wa Tanga, Dk. Edmund Mndolwa, ameahidi kuinua uchumi wa Mkoa wa Tanga kupitia kilimo cha biashara ili kuwakomboa vijana kiuchumi.
Akizungumza wakati wa kujifunza kilimo cha biashara katika Kata ya Kwadelo, wilayani Kondoa, alisema elimu aliyoipata ataipeleka mkoani Tanga ili vijana wa mkoa huo nao waweze kunufaika.
Mndolwa ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC), aliongozana na madiwani wawili akiwamo Diwani wa Kerenge, Shebila Iddi na Diwani wa Mnyazi, Muhidin Rajabu, ambapo walitembelea shamba la Halima Selemani lenye ukubwa wa ekari 60 lililokuwa limelimwa alizeti.
Diwani wa Kwadelo, Omary Kariati, alisema wananchi wakipewa elimu juu ya matumizi ya kitu chochote chenye masilahi ya maisha yao huitikia kwa haraka na hatimaye maendeleo hujitokeza.
“Katika kata yangu wananchi wamejitahidi kujitoa katika kilimo na kuhakikisha wanaondokana na tatizo la njaa kwa kila mwaka kupitia mradi wa Kilimo Kwanza,” alisema Kariati.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269