Breaking News

Your Ad Spot

May 22, 2013

KINANA KUMBURUZA MAHAKAMANI MBUNGE PETER MSIGWA


DODOMA, Tanzania
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, amempa siku 21, mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (pichani) kuomba radhi kwa madai yake kwamba kiongozi huyo (Kinana) amehusika katika usafirishaji wa pembe za ndovu, vinginevyo atamburuza mahakamani.

Kufuatia dhamira hiyo, Wakili wa Kinana, Eric S. Ng'maryo kwenda kwa Msigwa.

Kwa mujibu wa barua hiyo ya Mei 14, 2013, ambayo Nkoromo Blog imepata nakala yake, tuhuma hizo dhidi ya Kinana kutoka kwa Mbunge huyo ni za uongo na zenye kumkashifu, kumfedhehesha na kumshushia hadhi.

Barua hiyo inaeleza kwamba Msigwa alitoa matamshi hayo mchana wa Aprili 21, 2013 katika mkutano wa hadhara wa kisiasa uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani, Wilayani Nyamagana jijini Mwanza.

Barua hiyo inanukuu maneno ya Msingwa akisema "...Kinana meli zake ndizo zinahusika na kubeba mape,mbe nchi hii, Kwa siku katika nchi hii tembo 67 wanauawa."

Barua hiyo inazidi kumueleza Msigwa kwamba; "Umeshatamka maneno haya au, yanayofanana na haya, katika hotuba zako nyingine nje ya Bunge, katika hotuba hizo na ile ya Mwanza, uliahidi kuzungumza zaidi uwapo bungeni:

"Nia ya ahadi hiyo ilukuwa kunoa hamu ya umma kufuatilia zaidi tuhuma zako dhidi ya Ndugu Kinana na pia kujaribu kujificha kwenye kivuli cha kinga ya  Bunge; mambo yote mawili yakiwa ni matumizi maovu na mabovu ya nafasi yako ya kisiasa na ya ubunge.

IFUTAYO NI BARUA YA WAKILI WA KINANA KWENDA KWA MSIGWA




No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages