Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Afrika, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo wa 14 wa baraza la usimamizi wa Mawasiliano Afrika, uliofunguliwa leo Mei 21, 2013 kwenye Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam

Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza
na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Mkoma, wakati akiondoka kwenye chumba
cha mkutano baada ya kufungu rasmi mkutano huo wa 14 wa baraza la usimamizi wa
Mawasiliano Afrika, uliofunguliwa leo Mei 21, 2013 kwenye Hoteli ya Double Tree jijini
Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Rais Tanzania Bara, Dk. Mohammed Gharib Bilal, ameitaka
sekta ya mawasiliano nchini kuhakikisha inakomboa wananchi kiuchumi,
afya,kilimo na kielimu.
Bilal alisema kuwa huduma za kibenki na kutuma fedha zitasaidia
kuondoa daraja lililokuwepo kati ya vijiji na mijini kutoka na huduma hizo
kutumia mtandao ya simu.
Akizungumza leo katika ufunguzi wa mkutano wa 14 wa baraza la
mawasiliano Afrika Dk. Bilal, alisema kuwa Serikali itahakikisha inatoa afya bora,
maji salama ya kunywa na usafi wa mazingira, elimu, chakula na malazi,
Pia alisema kuwa itahakikisha inaboresha afya ya uzazi na
kupunguza vifo vya watoto wachanga, kuwawezesha wanawake na wananchi wenye
mazingira magumu zaidi ya jamii na kuhakikisha kunakuwepo na mazingira endelevu.
Dk. Bilal alisema mawasiliano ya makampuni katika Afrika yakifanya
kazi kwa pamoja yatasaidia kuinua watu waishio vijijini na kutoa huduma bora ikiwemo
kurahisisha upatikanaji wa mawasiliano na huduma za mtandao.
Mkutano huo umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), na kuhudhuriwa na waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Prof Makame
Mbarawa na Mawaziri wa mawasiliano kutoka Sudan na Ghana.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269