Breaking News

Your Ad Spot

May 17, 2013

RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE ATEMBELEA KIWANDA CHA EAST COASTS OILS AND FATS KAMPUNI TANZU YA METL IKIWA NI KAMPENI YA KUHAMASISHA LISHE BORA NCHIN


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb) wakati wakisubiri kuwasili kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL kuhamasisha Lishe Bora kwa walaji kwa kuongezaji Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani yakiwemo mafuta ya kupikia.
Picha juu na chini Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wafanyakazi wa Kiwanda ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL wakisubiri kumpokea Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha Lishe Bora kwa walaji kwa kuongezaji Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani yakiwemo mafuta ya kupikia.
Wafanyakazi wa Kiwanda ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL wakisubiri mkumpokea Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha Lishe Bora kwa walaji kwa kuongezaji Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani yakiwemo mafuta ya kupikia.
Picha juu na chini ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb), akimlaki Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili Katika Kiwanda cha East Coasts Oils and Fats ambacho ni Kampuni Tanzu ya MeTL. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq.
Afisa Mwajiri wa kampuni ya East Coasts Oils and Fats ambayo ni Kampuni tanzu ya MeTL Bw. Eric Buberwa akisalimana na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika kampuni hiyo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kusalimiana na wadau mbalimbali wa masuala ya Lishe.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb), akiteta jambo na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wakielekea sehemu ya kiwanda cha East Coasts Oils and Fats. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL Bw. Vijay Raghavan akifafanua jambo kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kukumimina Virutubishi vya Vitamini A katika Kinu cha kuzalisha mafuta kiwandani hapo ikiwa ni ishara ya kuhamasisha Lishe bora kwa walaji.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimimina mafuta ya virutubishi katika kinu cha kutengeneza mafuta ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kampeni ya kuhamaisha Lishe bora kwa walaji kwa kuongezaji Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani, wakati alipotembelea Kiwanda cha EAST COAST OILS & FATS ambacho ni kampuni tanzu ya MeTL kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Wanaoshihudia tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq (kushoto), Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL Bw. Vijay Raghavan ( wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb) (wa tatu kushoto) pamoja na wadau wengine wa masuala ya Lishe.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats ambayo ni Kampuni Tanzu ya MeTL Bw. Vijay Raghavan akitoa maelezo kwa Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete ya namna wanavyopima mafuta yao kwa Teknolojia ya Kompyuta wakati Rais Dkt. Kikwete alipotembelea kiwanda hicho kuhamasisha Kampeni ya Uongezaji wa Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani ili kutengeneza Lishe bora kwa walaji. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb).
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb) akifafanua jambo kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipotembelea kiwanda cha East Coasts Oils and Fats ambacho ni kampuni tanzu ya MeTL.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wafanyakazi wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL mara baada ya kumaliza zoezi la kutembelea kampuni hiyo inayozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mafuta ambapo amempongeza Mh. Mohammed Dewji kwa kutengeneza ajira kubwa kwa Watanzania kupitia kiwanda chake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL wakimsikiliza Mh.Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya MeTL pamoja na wadau wa masuala ya lishe alipotembelea Kiwanda cha East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL katika Kampeni ya Uongezaji wa Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq, Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb), Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema kwenye picha ya pamoja na wadau wengine wa masuala ya Lishe.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb) (kushoto) mara baada ya kuhutubia wafanyakazi wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq na mdau wa masuala ya lishe.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb), akiagana na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumaliza ziara yake katika kiwanda cha EAST COAST OILS & FATS ambacho kampuni tanzu ya MeTL ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Lishe bora kwa walaji kwa kuongezaji wa Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani.  (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages