.

MAJOGOO YAZIPIGA KAWE, DAR ES SALAAM, LEO

Jun 28, 2013

 Jogoo wakipambana katika eneo la Mbezi Beach, Kawe, Dar es Salaam. leo. chanzo cha ugomvi huo uliodumu kwa zaidi ya dakika tano kabla ya kuamuliwa na wapitanjia hakikuweza kujulikana mara moja.
 2
 3
 4
 5
 6
 7
 8
 9
 10
 11
 12
 PICHA ZIMEPIGWA NA KUTAYARISHWA NA: NKOROMO BLOG

MAANDALIZI UZINDUZI KIVUKO CHA Mv CHATO


Fundi akiandaa bango la uzinduzi wa Kivuko cha Mv Chato mkoani Kagera, kama alivyokutwa na mpigapicha wetu eneo la Mnazi Mmoja jijini Dar e3s Salaam, leo. Kwa mujibu wa fundi huyo bango hilo litasafirishwa kwa ndege kwenda huko Chato! Swali tunalojiuliza ni je huko Kagera hakuna wachoraji??????

OBAMA'S VISIT: BUSINESS LEADER CALLS FOR RULES OF ENGANGEMENT WITH AFRICA TO CHANGE

heirs-holdings.JPG

Elumelu says Africa open for business, but not at any cost
LAGOS, Nigeria,
Tony-Elumelu_.JPG
Tony Elumelu
June 28, 2013-- On the eve of his departure to Dar es Salaam, Tanzania, as part of a delegation of high profile African business leaders handpicked by the White House to meet with President Obama, Tony O. Elumelu, chairman of one of the most diversified investment groups in Africa, reiterated his message for the United States and international investors to engage proactively with Africa's private sector to develop the continent. 

In a wide ranging interview (available for download at AllAfrica.com), Elumelu talked about the rules of engagement for Africa having changed and that those looking to invest on the continent should consider aligning with an economic philosophy he called Africapitalism. The concept seems to be gaining momentum on the continent and beyond - the UK Guardian newspaper yesterday ran a feature suggesting it could be the new model for Africa’s development.

"Africa's economic history has been characterised by extractive industries and rent seeking practices that have not created development in any meaningful way. Africapitalism is simply saying there is a better and more ethical way to invest in Africa for a sustainable future. I would like to see both African and international investors review their strategies for Africa. Yes, we are open for business but not at any cost. Our rules of engagement have changed,” said Elumelu.

It is anticipated Elumelu will be part of a major announcement the US government will make about the power sector. Through Transcorp, one of Heirs Holdings investee companies, the group recently invested USD300 million in Nigeria's largest power plant, located in Ughelli, Delta State during the Nigerian government's recent power privatization process.

Commenting on the motivation behind the power investment, he said, "Unlimited access to affordable power in any country is a game changer and will move the needle on the country's development exponentially."

Elumelu continued, "It's not just the fact that children will be able to do their homework, or that computers and phones can be powered in rural villages; it is also the impact that access to affordable power will have on the economic ecosystem. Prices will come down, entrepreneurs will expand and innovate, and jobs will be created as a result. This is Africapitalism at work."

Other investments aside, Elumelu has been vocal about power, which has led many to speculate that Elumelu is looking to make a significant impact in this sector, much as he did in banking during his time as the Group CEO of UBA.

“We played a transformative role in democratizing the banking sector at a time when no one was really paying much attention to Africa, Elumelu says. “We had a clear strategy, first mover advantage and an understanding of what the market needed and we are focused on doing the same for power. We are taking over an old government-run plant that desperately needs rehabilitation and doubling its output within our first two years of operations. By 2017, we will be generating 1000MW of electricity and Nigerians across the country will feel the impact of affordable and consistent power."

Distributed by the African Press Organization on behalf of Heirs Holdings.


Download the full Tony O. Elumelu interview here at http://allafrica.com/stories/201306271650.html?viewall=1.

Read the UK Guardian article here: http://www.guardian.co.uk/global-development/2013/jun/26/africapitalism-african-self-empowerment

Media contact:
Moky Makura
Director, Marketing & Corporate Communications
Heirs Holdings
moky.makura@heirsholdings.com  
+234 1 277 4641-5

PINDA AKUTANA RAIS MTENDAJI WA KAMPUNI ILIYOGUNDUA GESI MTWARA

Jun 27, 2013


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Bw. Lars Christian Rais Mtendaji wa STATOIL kampuni ambayo imegundaua gesi katika maji ya bahari yenye kina kirefu katika eneo la Mtwara, bungeni mjini Dodoma Juni 27, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)

MAMA PINDA AZAWADIWA NA WANANAWAKE TOKA BUTIAMA

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akifurahia zawadi ya kitenge aliyozawadiwa na wanawake  kutoka wilaya ya Butiama mkoani Mara katika chakula cha jioni alichowaandalia kwenye hoteli ya New Dodoma mjini Dodoma June 25,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS KIKWETE AMPOKEA RAIS SRI LANKA, AKUTANA NA KIONGOZI WA UNDP LEO

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuweasili nchini  kwa ziara ya kikazi leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Kiongozi wa Shirika la UNDP(UNDP Administrator) Bi. Helen Clark ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.(picha na Freddy Maro).

OFA YA 77 KWA MA-BLOGGER

Inline image 1
                     _________________________________
For all your Blog and social media needs visit Blogintz a freelance consulting outfit specializing in providing solutions for Blogs including setup, management, analysis, optimization, social media etc. 
Visit us by clicking HERE to see how we can be of service.

                           _____________________________________________

TAMASHA LA WASANII MKURANGA LAAHIRISHWA KUPISHA MAPOKEZI YA OBAMA

Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la Mastaa Chipukizi lililokuwa lifanyike Jumamosi Juni 29 kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga limeahirishwa ili kutoa nafasi kwa  wasanii na viongozi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi ya  Rais wa Marekani, Baraka Obama (pichani).
 
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caaasim Taalib alisema jana kuwa wanachama wengi waliokuwa washiriki tamasha hilo watakuwa katika maandalizi ya ujio wa Rais Obama hivyo litafanyika mwezi Agosti baada ya sikukuu ya Idd el Fitri.
 
Taalib alisema anawaomba radhi wananchi wa Mkuranga, viongozi mbalimbali na wasanii washiriki wa tamasha hilo waliokuwa wamejiandaa kuonesha vipaji vyao katika tamasha hilo.
 
‘Tumeamua kutoa nafasi hii kwa wanachama wa SHIWATA ili washiriki kikamilifu kudumisha amani katika wakati huu ambao tunatembelewa na Rais Obama na wasanii washiriki kikamilifu, tunaomba tutoe taarifa katika vyombo vya dola mara tunapoona kuna unjifu wa amani’ alisema Taalib. 
 
Mwenyekiti huyo alisema mgeni rasmi aliyekuwa ameandaliwa, Naibu Waziri wa Kilimo, Adam Malima amepelekewa ujumbe huo pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wabunge wa Dar es Salaamnao wamearifiwa kuhusu kusogezwa mbele tamasha hilo.
 
Alisema sambamba na tamasha hilo, SHIWATA ilikuwa ikabidhi nyumba kwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jellah Mtagwa na wasanii wengine 14 ambao wamekamilisha michango ya ujenzi  wa nyumba zao katika kijiji chao cha Mwanzega Kimbili, Mkuranga.
 
Wengine watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu nchini, Lumole Matovola ‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni wanachama wa SHIWATA wangine ni Mwandishi wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la Magereza, Flora Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).  
 
 Mpaka sasa SHIWATA imejenga nyumba 24 kwa ajili ya wasanii katika eneo la hekari 300 na wanajiandaa kulima shamba la hekari 500 walizonazo ili kujikwamua kimaisha.

UNIC,TAYODEA WAANDAA SEMINA KUPIGAVITA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA TANGA

_DSC1238
Picha juu na chini ni Afisa uhusiano wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akiwasilisha ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya kwenye kongamano la vijana kuhusu madawa ya kulevya mjini Tanga.
_DSC1214
_DSC1161
Afisa habari wa kituo cha taarifa cha Umoja wa mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akikabidhi Beji ya utambulisho kwa mmoja wa vijana aliyekaa miezi sita kwenye nyumba ya mafunzo ya waathirika wa madawa ya kulevya bila kutumia madawa hayo mjini Tanga katika kituo cha Tanga Sober House.
_DSC1215
Pichani juu na chini ni baadhi ya vijana wakifuatilia semina ya kupinga matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya iliyoandaliwa na Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa kushirikiana na TAYODEA.
_DSC1215
_DSC1179
Ujumbe kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa Dar es Salaam, waandishi wa habari na watumiaji wa dawa za kulevya walioonyesha nia ya kuacha kutumia dawa hizo mjini Tanga, ambao wapo kwenye nyumba ya mafunzo ya kuwawezesha kuachana na dawa hizo (TANGA SOBER HOUSE) iliyopo Tanga. Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara ya dawa za kulevya ambayo hufanyika 26 June kila mwaka. Kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika mjini Dodoma.

MTEMVU NDANI YA TEMEKE

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (aliyevaa miwani katikati), akifuatwa na wananchi baada ya kumaliza mkutano wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimsikiliza Mweka Hazina wa Kikundi cha Kuweka na Kukopa (VICOBA), Anjela Ndigula ambaye alipokea sh. 50,000 alizotoa msaada kwa Muya Thabit ili ajiunge na kikundi hicho, baada ya kuambiwa hana haki hivyo anashindwa kulipia pango. Msaada huo aliutoa katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
 Muya Thabit akicheza kwa furaha baada Mbunge Mtemvu kumsaidia fedha za kujiunga na vicoba
 Diwani wa Kata ya Temeke, Khamis Nsombo, akiwazawadia fedha wasanii wa kikundi cha Msimamo

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akikizawadia fedha kikundi cha sanaa cha Msimamo kilichokuwa kinatumbuiza katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. Pia aliahidi kukipatia kikundi hicho sh. 500,000 za kununulia vifaa zikiwemo ngoma.
 Mtemvu akiangalia wakati msanii wa Msimamo akicheza ngoma
                             Wasanii wakicheza ngoma ya Lizombe ya asili ya Mkoa wa Ruvuma
                                             Msanii akichangamsha mkutano huo
                         Mtemvu akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Temeke, Khamis Nsombo
                                              Nsombo akiteremka kutoka jukwaani baada ya kuhutubia
                                                       Mtemvu akiwasalimia wananchi
                           Muya Thabit akiomba fedha kwa Mbunge Mtemvu ili alipe pango
                                    Wananchi wakiuliza maswali kwa Mbunge wao Mtemvu
ILO NA TACAIDS WAENDESHA KONGAMANO LA KUJADILI MIKAKATI YA KUWAWEZESHA WANAWAKE, WASICHANA NA WAVULANA KIUCHUMI KATIKA HARAKATI ZA KUPUNGUZA HALI HATARISHI ZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI NCHINI.

Jun 26, 2013

IMG_2657
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo amesema kupitia msaada kutoka Serikali ya Sweden wa kifedha ILO iliweza kuwahusisha wasichana na wavulana katika makundi mbalimbali wenye vipato vidogo kupata uelewa wa Afya ya Uzazi kupitia Makongamano, Semina na Mafunzo mbalimbali yaliyoendeshwa na shirika hilo la kazi Duniani.
Ameongeza kuwa “tuliwasaidia kuwaunganisha na vikundi vya kuweka na kukopa ili waweze kupata mitaji midogo midogo ya kufungua biashara ndogo ndogo katika harakati za kuwafanya wajitegemee na kuepekana na vishawishi vya Ngono isiyokuwa Salama.
Bw. Musindo amesisitiza Umuhimu wa TACAIDS kuandaa makongamano kama haya ili kuwawezesha wasichana na wavulana wadogo kupata ufahamu uelewa na mafunzo ya uzazi wa Afya na jinsi ya kuelewa mabadiliko yao ya kimaumbile.
“Ni matumaini yangu mwingiliano huu wa Utamaduni wa kupambana na Ukimwi, Kinga na Uwezeshwaji wa Kiuchumi umefanyika vizuri, hasa katika kuyalenga makundi yaliyo katika mazingira magumu itasaidia kuongeza kasi ya kupunguza maambukizi mapya kama ilivyoripotiwa na ripoti ya UNAIDS mwaka 2012 Duniani kwamba maambukizi mapya yamepungua kwa Asilimia 20”. Amesema.
IMG_2710
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo kwenye Kongamano hilo.
IMG_2731
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi Mtengwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo amesema mikakati ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi inaweza kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake, Wasichana na Wavulana wadogo.
Amesema Jamii lazima itambue kuwa juhudi zaidi zinahitajika ili nchini yetu iweze kufikia malengo ya 0.3 yaani Tanzania ambayo haina maambukizi mapya ya VVU, Ukimwi usiwe sababu ya vifo, vile vile pasipo unyanyapaa wala ukatili kwa mtu yeyote anayeishi na Virusi vya Ukimwi.
IMG_2702
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho akizungumza na washiriki amesema Takwimu zinazonyesha Wanawake wako katika hali ya hatari ya kuambukizwa zaidi kuliko wanaume ambapo mpaka sasa ni Asilimia Sita ya Wanawake nchini huambukizwa wakati wanaume ni Asilimia 3 nchini nzima.
Dr. Mrisho alisisitiza umuhimu wa kumwezesha mwanamke kiuchumi kama ndio moja ya suluhisho la kumfanya kutokuwa tegemezi katika jamii.
“Amesema takwimu zinazonyesha katika nchi nyingi za Kiafrika umaskini unachagia sana kuenea kwa Ukimwi maana Wanaume wengi hutumia umasikini wa Wasichana au Kinadada kuwarubini kwa fedha na kufanya nao Ngono isiyosalama”.
Dr. Fatma Mrisho amepongeza juhudi za ILO na kuwataka mashirika mengine na wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi kuiga juhudi zilizofanywa na ILO za kuandaa makongamano ya kiuchumi ili kumwezesha Mwanamke na wavulana wadogo kujitambua na kuelewa jukumu lao katika mapambo ya VVU na Ukimwi nchini.
IMG_2737
Meza Kuu: Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi Tanzania (UNAIDS) Dr. Hedia Belhadj, Mwakilishi kutoka TUCTA Bw. Hezron Kaaya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi Mtengwa, Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo, Mkurugenzi wa Sera na Utetezi wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) Bi. Justina Lyela.
IMG_2723
Mwakilishi kutoka shirikisho la wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Hezron Kaaya alisisitiza mshikamano na umoja wa wafanyakazi katika mapambano ya VVU na Ukimwi sehemu za kazi.
Bw. Kaaya amesisitiza majadiliano kama hayo yasiishie kwenye makabrasha bali wayatekeleze kwa vitendo ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii.
IMG_2721
Mkurugenzi wa Sera na Utetezi wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) Bi. Justina Lyela akitoa nasaha zake kuhusu viwango sawa vya malipo ya mishahara kwa wafanyakazi nchini ili kuwakomboa wanawake na kipato kidogo makazini.
IMG_2709
Picha juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchini wa Kongamano la kuwawezesha Kiuchumi Wanawake, Wasichana na Wavulana dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi lililofanyika leo jijini Dar na kuratibiwa kwa pamoja kati ya ILO na TACAIDS.
IMG_2632
IMG_2654
IMG_2741
Washiriki wa Kongamano hilo wakiangalia baadhi ya machapisho mbalimbali ya VVU na Ukimwi.
IMG_2745
Picha juu na chini mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo la siku moja lililofanyika jijini Dar es Salaam.
IMG_2758
ยช