Breaking News

Your Ad Spot

Jun 18, 2013

KINANA:CCM HAITADHOOFISHWA KWA KUSINGIZIWA MABAYA YA WENGINE

KINANA
NA SHAABAN MDOE,ARUSHA.
KATIBU Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amesema ndoto za viongozi wa Chadema kuwa watakidhoofisha CCM kwa kukisingizia kuhusika na mlipuko wa bomu Arusha na wenyewe kujiimarisha kwa kutumia misiba ni ndoto za mchana kweupe.

Kinana ametoa kauli hiyo leo alipokua akizungumza na Uhuru katika hospitali ya KKKT ya Selian jijini Arusha alipofika kwaajili ya kuwajulia hali majeruhi wa tukio la kulipuliwa kwa bomu wakia katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani wa Chama Cha Demokrasi na Maendelo Chadema Soweto kata ya Kaloleni jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

Katibu mkuu huyo alisema kamwe Chadema haitapata umaarufu wa kisiasa kwa kuteka misiba ya kiaifa na kuifanya yakwao kwakua kipindi cha kuendelea kuwadanganya wananchi wa Tanzania kimekwisha  na wako mbioni kuumbuka kutokana na matukio hayo.

Aliwataka viongozi wa Chadema kuacha kutumia misiba hiyo kujinufaisha kisiasa kwa kuwatuhumu watu au vyama vingine vya siasa na badala yake kuviachia vyombo vya dola kuifanya kazi yao kwakua wao ndiyo pekee wanoweza kujua undani a tukio hilo na sio wao.

Aidha aliwataka viongozi hao kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kufanikisha kupatikana kwa wahalifu wa tukio hilo ili kuwzesha kumaliza kabisamatukio hayo yaliyojitokeza katika mkoa wa Arusha tena katika vipindi vifupi vifupi na kusababisha vifo na majeraha kwa wananchi.

Hata hivyo Kinana alisema hana wasiwasi juu ya kauli ya serikali kupitia viongozi wake kuhusu kufuatilia jambo hilo kwa kina kwakua uwezo wanao pamoja na sababu ikiwa ni kuweka hali ya usalama na amani idumu katika mkoa wa Arusha na vitongoji vyake na hata nchi kwa ujumla.

Alisema dhamira iliyopo kwa serikali ni kutambua wakina nani waliofanya jambo hilo kwa kutumwa na akina nani pamoja na sababu ya kufanya hivyo jambo ambalo linapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania anayeipenda nchi yake badala ya kubaki kutupiana lawama juu ya tukio hilo baya.

Alisema chama chochote cha siasa kinapaswa kuonyesha masikitiko katika tukio hilo badala ya kuwatumia wananchi kuendelea kuvunja sheria kwa kufanya maandamano yasiyo na msingi kwakua kinachopaswa kufanyika ni kuwahamasisha wananchi kutulia na kutoa ushirikiano wa tukio hilo ili kuwapata wahalifu.

Kinana alitumia pia nafasi hiyo kuwapa pole wale wote waliofiwa na ndugu zao katika tukio hilo,kuwatakia wapone haraka majeruhi wote wa tukio hilo pamoja na kuipongeza serikali na madaktari na wauguzi wa hospitali mbalimbali mkoani Arusha kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuwauguza majeruhi wa tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages