Breaking News

Your Ad Spot

Jun 11, 2013

MTEMVU ATOA MSAADA WA SH. MIL 3.5 KWA VICOBA, ULINZI SHIRIKISHI

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alivikabidhi vikundi vitano vya Kuweka na Kukopa (VICOBA, kila kimoja msaada wa sh. 500,000 na kikundi cha ulinzi shsirikishi sh. 500,000 za kutunisha mifuko hiyo.

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akikumbatiana na mmoja wa wanachama wa kikundi cha Vicoba cha Tuyangatane waliofurahi kupatiwa msaada wa sh. 500,000 za kutunisha mfuko wa kikundi hicho.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Wanachama wa Tuyangatane wakifurahia kupata hundi hiyo.

 Mtemvu akikipatia kikundi cha Vigoba cha Tumaini msaada wa sh. laki tano

 Kikundi cha Tupendane kikipatiwa laki tano



 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), kulia, akimkabidhi hundi ya sh. 500,000 Mweka Hazina wa Kikundi cha Saccos cha Pambazuko, Sophia Said, kwa ajili ya kutunisha mfuko wao, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alivipatia pia kiasi kama hicho vikundi vingine vitano.

 Mtemvu akimvisha filimbi Juma Mlanzi ambaye ni miongoni mwa walinzi shirikishi  56 waliohitimu mafunzi ya kijeshi. Pia walikabidhiwa vyeti.

 Juma Kambona akikabidhiwa cheti baada ya kuhitimu mafunzo hayo

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), wa pili kulia, akimpatia cheti Mwanaisha Gea ambaye amekuwa miongoni mwa vijana 56 waliohitimu mafunzo ya Ulinzi Shirikishi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alikikabidhi pia kikundi hicho cha Ulinzi Shirikishi sh. 500,000 za kuanzishia Saccos yao. Kulia ni Diwani wa Kata ya Azimio, Hamis Mzuzuri.

 Jumanne Jumbe naye akikabidhiwa cheti baada ya kuhitimu mafunzo hayo

 Mma Mkazi wa Kata ya Azimio akilalamika mbele ya Mtemvu, kuhusu mchezo wa Kangha Mbendembende au kangamoko unavyowadhalilidha wanawake ambapo aliomba upigwe marufuku kwa vile auendani na maadili ya kitanmzania.

Mgambo Said Amiri akilalamikia kitendo cha mabosi wake wa Kituo cha Polisi cha Tambuka Reli kinavyowalea vibaka na majambazi katika eneo hilo.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages