Breaking News

Your Ad Spot

Jun 2, 2013

WAKUVWANGA AISAMBAZA ALBAMU YA 'KATO'


Na Elizabeth John
MSANII kutoka kundi la Orijino Komedi, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ ameachia albamu yake ya kwanza inayojulikana kwa jina la ‘Kato’ ambayo imeanza kufanya vizuri katika soko la muziki.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wakuvwanga alisema nyimbo ambazo zipo katika albamu hiyo, zimechanganyika alizoimba kwa lugha ya kinyakyusa na zingine ameimba Kiswahili.
“Mimi ni Mnyakyusa nimeamua kuimba kwa lugha hiyo ili hata wenzangu waliopo Mwakaleli waelewe nimeimba nini, naamini itafanya vizuri sokoni,” alisema Wakuvwanga.
Wakuvwanga aliwataka wadau wa muziki nchini wampokee katika tasnia hiyo na kuwaahidi kuwaletea vitu vizuri zaidi ya hivyo, mbali na kwamba yeye ni msanii wa maigizo.
Wasanii wengine ambao wanaunda kundi hilo la Orijino Komedi ni pamoja na Joti, Mpoki, Masanja, Vengu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages