Breaking News

Your Ad Spot

Jul 23, 2013

BALOZI ZA EU ZADAIWA KUWAKWAZA WATANZANIA WANAPOOMBA VISA KWENDA KATIKA NCHI ZA ULAYA

Imedaiwa kwamba Balozi za  nchi za Ulaya zilizopo Tanzania ambazo ni pamoja na Balozi za Ujerumani, Ubelgiji na Netherland zimekuwa zikiwasumbua sana raia wa Tanzania wanaohitaji Visa za kusafaria kwenda katika nchi za hizo.

Malalamiko yaliyoufikia mtandao huu, yanadai zaidi kwamba pamoja na Watanzania kutimiza masharti yote yanayohitajika katika kuomba Visa lakini balozi hizo zimekuwa bado zikiwawekea vikwazo visivyo katika sheria za maombi ya Visa.

"Mfano Mtanzania anapo omba Visa ubalozini atapeleka barua ya mwaliko na bima,pamoja na benk statment, barua ya kazini, pay insleep za mishaara, lakini eti bado afisa balozi anadai barua nyingine itoke kwa mwenyeji kuonyesha milijuana naye vipi? na mgeni Mtanzania!" ameeleza mlalamikaji na kuongeza;

"Kwa kweli hakuna uhusiano mzuri katika ya raia na maofisa wa visa wa balozi za EU nchini Tanzania. Watanzania wanapoomba Visa wanasumbuliwa sana sana hapa nchini. Serikali inaweza kuwa na uhusiano mzuri na balozi hizo lakini raia wa Tanzania hawathaminiwi kabisa na balozi za EU hapa Tanzania".

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages