Breaking News

Your Ad Spot

Jul 20, 2013

NAIBU MEYA SHINYANGA (CCM) ATETEA KITI TENA

NA CHIBURA MAKORONGO, SHY
UCHAGUZI wa Naibu meya  katika Manispaa ya Shinyanga umefanyika jana ikiwa Davidi Nkulila (CCM)  diwani kata ya Ndembezi amerudia kuongoza kiti hicho kwa kupata kura 14 zilizopigwa na wajumbe hao kati ya kura 22 huku mpinzani wake Nyangaki Shilungusheila  (CHADEMA) diwani kata ya Kambarage  akiambulia kura  nane
.
Katika uchaguzi huo  ulioongozwa na mstahiki meya  Gullamu Hafidhi Mkadamu  akiwepo na mkurugenzi wa manispaa hiyo Festo Kang’ombe uliofanyika   ndani ya ukumbi wa mkoa  mara baada ya kumaliza  kikao cha bara za la madiwani huku zikiundwa kamati mbili za kudumu.

Hata hivyo  kamati hizo ambazo ni  kamati ya afya,elimu,uchumi na fedha ambapo mwenyekiti wake Charles Njage ( CCM)diwani wa  kata ya Kizumbi alichaguliwa kwa kupigiwa kura na wajumbe waliokuwa ndani ya kamati hiyo.

Aidha katika  upande wa  kamati ya miundombinu mwenyekiti alichaguliwa Thomas Chuma (CCM)  diwani wa kata ya Lubaga  huku  wajumbe wengine wakiendelea  kuchaguliwa kuwemo ndani ya kamati mbalimbali zilizopo. 

Pia Nkulila aliwashukuru wajumbe kwa kumpatia kura za kurudi tena katika uongozi kwa nafasi hiyo na kuwaahidi ushirikiana kama alivyokuwa akifanya siku zote katika uongozi huo huku shilungushela akikubali matokea hayo.
 
Alisema katika uongozi wake hapendelei mambo ya siasa katika vikao vya kwenye baraza la madiwani  bali kinachotakiwa ni kuwa kitu kimoja cha kuwawakilisha wananchi matakwa yao walivyoyaagiza kuhusu siasa ni  nje mara baada ya kikao kumalizika.

Hata hivyo madiwani hao  walipongeza  uchaguzi huo ulikuwa wa uhuru na haki, ikiwa mwanasheria wa manispaa hiyo James Mwakinya akisoma vifungu vya kanuni na sheria vya  uchaguzi huo kuwa  uchaguzi huo ni wa haki  kwa kila mwaka kumpata naibu au makamu mwenyekiti ndani ya manispaa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages