Breaking News

Your Ad Spot

Jul 12, 2013

SHIGELLA: GREENGUARD YA CCM SIYO KAMA REDBRIGED INAYOTAKA KUANZISHWA NA CHADEMA

KATIBU MKUU WA UVCCM, MARTINE SHIGFELLA LEO AMZEZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NA KELEZA MAMBO MATATU MUHIMU LIKIWEMO HATUA YA CHADEMA KUTAKA KUANZISHA MGAMBO KINYUME CHA SHERI.
SASA FUATILIA MAELEZO HAYA KAMA YALAIVYOTAYARISHWA NA  ASENGA ABUBAKAR WA MAKAO MAKUU YA UVCCM

1.kuanzishwa kwa REDBRIGED ya chadema hakukubaliki, chadema lazima watofautishe kati ya vijana wa CCM ambao wanapewa mafunzo ya ukakamavu juu ya chama katika kueneza sera na kuandaliwa kama viongozi wa baadae na kikundi cha kijeshi kinachoanzishwa na wao kwa maana wanaosema ya kujilinda DHIDI YA POLISI

CCM haina kikundi cha kujilinda dhidi ya polisi au wanajeshi.UVCCM inavikundi kwa ajili ya ukakamavu wa vijana wake,je chadema hawatakuwa na haja ya kuwa na askar polisi kwenye mikutano yao?

so hilo tunalilaani na hatuliungi mkono

2.Tunataka vijana wetu toka kwenye mashina matawi ,kata na wilaya washiriki vyema kuwaaambia wajumbe wa mabaraza ya katiba maoni wanayoona yanafaa kwenye katiba mpya

hatuungi mkono ujio wa serikali tatu , gharama za serikali hizo ni mzigo kwa watanzania lakini pia mchakato wa kuleta serikali ya tatu haukubaliki,unawezaje leo upate mtoto wakati mzazi mmoja haujamtafuta?

inamana zanzibar wanakatiba yao, bara unasema hawana katiba yao eti itakuja baadae?

walipaswa kwanza waje na mapendekezo ya rasimu ya jinsi serikali ya zanzibar inavyopaswa kuwa katika serikali ya muungano

pili waje na mapendekezo ya katiba ya jinsi serikali ya bara itakavyokuwa

na mwisho waje na rasimu ya serikali ya muungano ili kila upande ujijue na si tuanze na serikali ya muungano alafu eti bara tuje tujijue baadae

PILI katika huo mchakato wa katiba kuna mambo mengi ambayo hayapo sawa,

mfano eti wanataka vijana wagombee ubunge wakiwa na umri wa miaka 25

hii si sawa,mimi nilizani wangesema kwa kuwa vijana wana haki ya kupiga kura wa kiwa na miaka 18, basi wawe na haki ya kugombea ubunge pia wakiwa na miaka hiyo hiyo.
Hao wajumbe wa katiba walipata uteuzi wa kuwa mabalozi nje ya nchi wakiwa na miaka 18 mfano dk salim A salim
sasa wanataka kuwachelewesha tu vijana ambao mtakubaliana nami kuwa sasa wamekuwa kiakili zaidi kuliko vijana wawakati ule wa analojia na wakati huu wa dijitali

na kwakuwa hakuna kijana aliegombea ubunge akiwa na chini ya maiaka 25 ameonyeshwa kushindwa majukumu yake basi tunaomba umri ubaki ule ule wa awali wa miaka21 au uwe miaka 18.

3. Mwisho kutakuwa na uchaguzi wa chipukizi taifa mwaka huu 2013 na fomu zinaanza kutolewa tar 5/7-30/07/2013 fomu zitatolewa mikoani,UVCCM zanzibar na UVCCM makao makuu zanzibar

nafasi zinazogombea ni

1.mwenyekiti wa chipukizi taifa nafasi 1
2.makamu mwenyekiti taifa nafasi 1
3.wajumbe wa wili wa baraza kuu taifa kutoka chipukizi nafasi moja bara na moja zanznibar
4. wajumbe wanne wakamati ya uendeshaji taifa wawili toka zanznibar na wa wili toka bara
5.wajumbe watatu wa mkutano mkuu wa UVCCM taifa chipukizi kwenda mkutano mkuu wa UVCCM Taifa ,nafasi mbili toka bara na nafasi moja toka zanzibar

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages