Breaking News

Your Ad Spot

Jul 30, 2013

WAZIRI MKUU WA THAILAND AANZA ZIARA YA KIKAZI TANZANIA, AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS JAKAYA KIKWETE, IKULU


  Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akikagua gwaride la heshima la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania mara baada ya kuwasili nchini Tanzania leo.
  Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania likipita mbele ya jukwaa kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kulia) na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiangalia vikundi vya ngoma akiwa na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete leo jijini Dar es salaam.
 Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania likipita mbele ya jukwaa kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kulia) na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo leo jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri mkuu wa Thailand ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand Dr. Surapong Tovichakchaikul (kushoto) na Waziri wa Fedha wa Tanzania Mh. William Mgimwa (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano ya kudumisha , kutunza na kuendeleza uwekezaji kati ya Tanzania na Thailand Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa Tanzania na Thailand walioongozwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Yingluck Shinawatra ambapo Tanzania na Thailand zimesaini mikataba minne ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa, uendelezaji wa shughuli za uwekezaji, ushirikiano katika masuala ya Ufundi na ushirikiano katika sekta ya Nishati na Madini. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages