Breaking News

Your Ad Spot

Aug 13, 2013

CCM YAWATOLEA UVIVU MADIWANI WAKE WANANE BUKOBA, YAWAVUA UANACHAMA, UONGOZI

BUKOBA, Tanzania
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuwatolea uvivu kwa kuwavua uanachama na uongozi madiwani wake wanane katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Imeelezwa kwamba hatua hiyo imechukuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kagera kutokana na madiwani hao kudaiwa kupuuza maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa na  Katibu wa CCM wa mkoa huo Avelin Mushi, na theNkoromo Blog kuipata, imesema kuwa uamuzi huo umekuja kutokana na chama kujali maslahi ya wananchi tofauti ya watu binafsi.

Mushi amewataja madiwani hao nane kuwa  Yusuph Ngaiza (Kata Kashai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Bukoba, Samwel Ruangisa (Kitendagulo) ambaye ni Meya mstaafu na Mkuu wa mkoa wa mkoa wa kwanza wa mkoa wa Kagera, Murungi Kichwabuta (Viti maalumu) Deusdedith Mutakyawa (Nyanga) Richard Gaspal (Miembeni)Alexander Ngalinda (Buhembe) ambaye pia alikuwa Naibu MeyaDauda Kalumuna (Ijuganyondo) na Robert Katunzi wa kata Hamugembe.

Mushi amesema kuwa  kufukuzwa kwa madiwani hao ni kutokana na mgogoro ulidumu kwa muda mrefu juu ya mbunge na meya ambapo Rais Kikwete akiwa ziarani Kagera alitoa agizo la wanachama hao kutoendelea na mgogoro huo.

Pia, amesema kuwa vikao vya chama vimekuwa vikiendelea kwa kufuata kanuni na taratibu kwa kuwaonya juu ya kuhujumu serikali ya CCM kwa kushirikiana na madiwani kambi ya upinzani kutotekeleza maendeleo ya wananchi lakini wahusika wote wamekuwa wakikahidi maagizo ya kuitwa kwenye vikao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages