Breaking News

Your Ad Spot

Aug 17, 2013

IMEDAIWA WENGI VIJIJINI HAWAJUI KINACHOENDELEA KUHUSU RASIMU YA KATIBA MPYA

SHINYANGA, Tanzania
Imeelezwa  kuwa  idadi kubwa ya watu wanaoishi vijijini  hawajui kinakoendelea katika rasimu ya Katiba mpya kutokana na sababu mbalimbali.

Hali hiyo inatokana na kwamba wengi wao hawajawahi kuiona rasimu ya katiba na waliobahatika kuipata wameitunza majumbani kwao bila kuifanyika kazi yoyote, sababu kubwa ikiwa ni kutokuwa na mwamko hivyo kukosa fursa ya kuchangia chochote katika la rasimu  hiyo.
 
Hayo yalielezwa katika mafunzo  yaliyo walenga walimu, viongozi wa dini pamoja na wakulima  kutoka shinyanga vijijini ilikuwajengea uwezo   wa kuichambuwa katiba iliwakatowe elimu kwa wenzao ambao hawakupata frusa ya kushiliki mafunzo hayo juu ya kuchangia maoni katika katiba.
 
Akieleza kuhusu mafunzo hayo  mkurugenzi wa  shirika la  Ulagabishaji {LDG} Jimmy Ruhende alisema kuwa lengo la shirika hilo nikuwapa uwezo wananchi ili waweze kuichambua katiba na kutowa maoni.
 
“ Wananchi waliowengi hawailewi rasimu ya katiba na waliobahatika kuioa bando hawajapata elimu ya kutosha juu ya kuisoma rasimu hiyo na kuichambuwa iliwaweze kutowa maoni badala yake huitunza tu, hivyo yunatowa elimui hii ili waamuke waweze kutoa maoni”alisema.
 
Hata hivyo mkurugenzi huyo alieleza kuwa mashirika yaliyo mengi yamekuwa yakieleza mafunzo hayo mijii na alioko vijijini kutopata fruza hizo, wameamuwa kujikita vijijini ili na wao waweze kuamka na kupata haki kama atanzania katika nchi yao .
 
Pia alisema kuwa kwasasa umma umegawanyika kutokana na wanasiasa mbao wamekuwa wakiwapotosha  wananchi na kuwaeleza masuala ya rasimu ya katiba kwa kwa matakwa yao ya kisiasa hivyo tunawapa elimu ili wajitambuwe wasipotoshwe na mtu yeyote.
 
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo walisema kuwa wanalishukuru  shirika hilo kwa kuwapa mafunzo ambayo yamewaamusha na kujitambu ambapo waliongeza kuwa kwasasa wanauwezo wa kutowa maoni yao bila woga wowowote.
 
“hatujawahi kuona katiba yoyote toka tuzaliwe lakini tumefulahi, na tunalishukuru shirika hili kwani nimala yetu ya kwanza kuiona rasimu na nimarayakwanza kushiriki vikao vya rasimu ya katiba hiyo hatuogopi kwasasa”walisema

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages